BAADA YA KUGOMA KUFUNGUA MADUKA WAKIGOMEA MASHINE ZA TRA..WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WAGOMEA SEMINA YA TRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyabiashara walio katika maeneo ya Kariakoo wamegoma kushiriki semina ya  uelimishaji iliyokuwa itolewe na  Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika kile walichokiita kupuuza madai yao na kutaka kufanya vile wanavyotaka wao kuhusiana na  sakata la mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato.
Mamlaka hiyo iliitisha mkutano katika Hoteli ya Starlight ikilenga kuwaelimisha wafanyabiashara hao juu ya matumizi ya mashine za kielektroniki, jambo ambalo lilizua zogo miongoni mwa  wafanyabiashara waliokuwepo katika eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wafanyabiashara wa nguo eneo la Kariakoo aliyekuwepo hotelini hapo, akijitambulisha kwa jina moja tu la Mwanahamisi alisema siku ya Jumatano gari la matangazo lilipita baadhi ya mitaa ya Kariakoo likiwataka wafanyabiashara hao wafike kwenye mkutano uliopangwa kufanyika.
“Kutokana na taarifa hiyo kuletwa kienyeji, baadhi ya wafanyabiashara wachache tumefika  tukijua tutapata ufumbuzi juu ya kilio  cha muda mrefu kuhusiana na malalamiko waliyopeleka kwenye mamlaka hiyo, a alisema.
Matokeo yake watu kutoka mamlaka hiyo waliofika kwenye mkutano, walianza kutoa utambulisho juu ya kile walichotarajia kukifanya ikiwa ni kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine hizo.

Gazeti la Mwananchi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad