MASOGANGE YUPO DAR..AJIFICHA KUKWEPA MAPAPARAZI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Gladness Mallya
VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye alipata soo la kukamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini amejaa tele jijini Dar es Salaam, Ijumaa limethibitisha.
Masogange akipozi na Jack Patrick.
Masogange ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward baada ya kunaswa na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni 4.8 ambapo aliweza kulipa na kuwa huru.
Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu, msanii huyo akawa hajulikani alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram zikionesha yupo Tanzania au Afrika Kusini.
Masogange akipozi dukani Bongo.
Jumatatu iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa simu na msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange akiingia kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke yake.
Paparazi wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo ambapo hata hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya kawaida.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.
Jack alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana, basi.”
Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange alipatikana na kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa sababu anawaogopa sana mapaparazi.
-Global Publishers
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Utamu wa dhambi huo sasa unaishia kujificha kama nyoka.

    ReplyDelete
  2. Sio kujificha hana hela tena, zile alizoringishia zimeisha! Ulimbuken hasara

    ReplyDelete
  3. kutaka maisha kiulaini ona sasa kama mkimbizi unayetakiwa kurudi kwenu.ukome mwanamke kama huyu ukioa unajichimbia kabuli.

    ReplyDelete

Top Post Ad