WEMA AIPASUA BONGO MUVI BAADA YA KUSUSIWA MSIBA WA BABA YAKE.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KLABU ya mastaa wa filamu jijini Dar es Salaam, Bongo Movie ‘Bongo Muvi’ imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Honorati Lasasi Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilio asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
LAWAMA ZOTE KWA RAY
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.

  
RAY AAGIZWA AITISHE KIKAO CHA DHARURA KUMJADILI
Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika wasanii wa Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.

NJAMA ZA KUINGAMIZA KABISA BONGO MUVI ZAUNDWA CHINI KWA CHINI
Habari zaidi kutoka kwenye kundi linalodaiwa kujimega kwenye mpasuko huo zinasema kuwa kuna njama za makusudi za kuiangamiza klabu hiyo kwa kuwa mbali na mwenyekiti huyo kuwazuia wajumbe wasiende msibani kwa mzee Sepetu lakini imekuwa ikiendeshwa kitemi na kibaguzi.
Ilisemakana kuwa kuna wasanii wameifanya klabu hiyo kama yao huku wengine wakiwa hawatakiwi hata kukohoa jambo walilosema si sawasawa.
“Kwa mpasuko huu, wasanii waliochukizwa na Ray wamesema nao wao wanakazia hapahapa, Bongo Muvi lazima iangamie moja kwa moja, isiwepo tena,” alisema msanii mmoja ambaye jina lake linapanda kwa kasi.
KISINGIZIO CHA WASANII WANAFIKI CHAPINGWA
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.
MAMA WEMA ASHTUSHWA
Akizungumza na waandishi wetu kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mwanaye alisusiwa msiba wa baba yake, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu alionesha kusikitishwa sana na kitendo hicho.
Alisema kitendo hicho kilitokea wakati ambao Wema au familia nzima ilikuwa inasaka faraja na si mfarakano kwa vile kufiwa kupo na hakuna dalili wala kujiandaa.
“Nilisikitika sana, lakini siwezi kusema mengi kwa sababu vijana wanataka mwongozo ili kwenda mbele, naamini watakaa na kuondoa tofauti zao,” alisema mama huyo mwenye mapenzi makubwa na mastaa wa filamu Bongo.
KATAZO LA RAY 
LILISIMAMIA HIVI
Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na Ray ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo walitaka na yeye amzike baba yake mwenyewe.
MISIBA ILIYOTOLEWA MFANO
Ulitolewa mfano msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.
MISIBA ALIYOSHIRIKI
Ilidaiwa kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wenzake, ikatolewa mifano misiba miwili aliyoshriki kuwa ni marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkiety) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.
ANACHOSIMAMIA WEMA
Akizungumzia tukio la kususiwa msiba wa baba yake, Wema alifunguka:
“Nimesikitishwa na kitendo hicho naamini hakikuwa cha haki, mimi nimekuwa nikihudhuria misibani kwa watu mbalimbali na si kweli kwamba niko kivyangu, nimehukumiwa bure.”
RAY AINGIA ‘PANGONI’
Juzi Jumanne, Amani lilimsaka Ray kwa njia ya simu ili aelezee ukweli wa madai hayo lakini aliingia ‘pangoni’ (hakupokea simu).
Hata hivyo, katika gazeti ndugu la hili, Ijumaa la Ijumaa, Novemba Mosi, 2013 ukurasa wa mbele ambapo kuna habari yenye kichwa; WEMA SEPETU ASUSIWA MSIBA, Ray aliulizwa kuhusu madai hayo ambapo alijibu:
“Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu, hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.”
Hakupiga.
MASTAA KIDUCHU MSIBANI
Pamoja na katazo hilo la Ray, wasanii wengine waliamua kwenda msibani Sinza – Mori (Dar) na wachache sana kwenye mazishi, Zanzibar.
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Jacob Stephen ‘JB’, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Salum Mchoma ‘Chiki’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na Jacqueline Wolper.
WASIOFIKA MSIBANI 
Wengi walimsusia msiba Wema, lakini majina makubwa zaidi wakiongozwa na Ray mwenyewe ni Single Mtambalike ‘Richie’, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, Irene Paul, Blandina Chagula ‘Johari’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ na Ruth Suka ‘Mainda’
Chanzo:GPL
-----------
Click like below

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ninachoelewa funzo kwa mtu asiyahudhuria misiba ya wenzie sio kumsusia msiba ila ni kwenda kwa wingi km aliyefiwa ana akili timamu atawaelewa tu hata bila kusemeshwa na njia nyingine ya kumrekebisha ni kwa mazungumzo sku hyo hiyo ya msiba,pole Wema ila naamini umepata funzo japo wenzio hawajatumia njia sahihi

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu kula tano

    ReplyDelete
  3. Bongo movie hv ilikuaje mkampa ray uongozi...? Hana elim c ya darasani tu hata elim dunia hana....talent ndo mavi matupu the guy hajui kuigiza totally kazi ni kupiga kelele tu,then mkampa uongozi...oneni anakowapeleka....leo hii jamii yote inawashangaa kwa mlicho kfanya,aibu yenu or yake...? Huyu jamaa matako kabisa..

    ReplyDelete
  4. Ukosefu wa elimu ni kitu kibaya mno!Hiyo sio njia ya kumfanya agundue kosa lake hata kama ni kweli haendi kwenye misiba ya wengine.Uongozi anatakiwa apewe mtu ambaye ana upeo mkubwa wa kufikiri na kufanya maamuzi,kwa hapo Ray umechemka!Jirekebishe hatuishi hivyo!

    ReplyDelete
  5. Kumbe Ray ni Bomu kabisa; ndiyo maana hata wakati wa msiba wa Kanumba alikuwa akiongea pumba tupu kwenye TV. Swala la kwenda msibani ni uamauzi wa mtu binafsi, siyo uamuzi wa chama au kilabu. Kama kiongozi mwenye busara atazuiaje watu binasfi wasiende misibani? Kama alikuwa hataki kilabu yao ishiriki basi angefanya hivyo kwa kukaa kimya na kutokuwa na representatio ya kilabu hiyo, lakini akawaacha wanachama wake kila mtu kivyake vyake. Hivi yeye anataka Bongo muvi itawale maamuazi binafsi ya wanachama wake pia?

    ReplyDelete
  6. Ila wasanii mnatabia mbaya cz dawa ya mtu asiehudhuria misiba ya wenziie ni kutozwa fain na co vinginevyo hta katika jamii ndo kinafanyika icho

    ReplyDelete
  7. huyo Ray angeshuhulikia afya yake kwanza n akutubia katika siku zake zilizobaki duniani kwa magonjwa sugu alokuwa nalo lakini bado ndo kwanza nalaanika na dunia. mi nilidhani kauli hiyo ilitoka kwa mwanamke kama uwoya kukataza watu wasiende msibani kumbe dume zimaaa lina safura kama anaeingia kwenye siku zake vile na yeye

    ReplyDelete
  8. Bongo Muvi wajinga wote

    ReplyDelete
  9. Haki ya nani mi nilijua hizo msg zimesambazwa na mwanamke ili watu wasiende msibani, Kumbe ni Ray?nimemshusha thalami Huyu mwanaume Kama mabinti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sorry ni thamani,huna busara kabisaaaaaa,ndio maana ulikuwa humpendi marehemu kanumba,wivu hata Wanaume ?

      Delete

Top Post Ad