AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Dk Msafiri alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kituo hicho ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa wanawake wanaopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kulawitiwa.
Alisema kituo hicho kinatumika vibaya kinyume na malengo yake ambapo wazazi wanawalazimisha watoto wa kike kuchunguzwa bikira yao baada ya kuwatilia shaka kwamba wanayo mahusiano ya kimapenzi na wanaume.
“Kituo hiki Mkono kwa Mkono malengo yake ni kutoa huduma za dharura kwa wanawake wanaokabiliwa na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa.....sasa wazazi wanawaleta watoto wao hapa baada ya kuwatilia shaka kwamba wanamahusiano ya kimapenzi na wanaume kwa ajili ya kuchunguzwa kujua ubikira wao,” alisema.
Alisema huo ni aina mpya ya udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu wanawake wengi wanapinga kuchunguzwa ubikra huo ambapo kazi hiyo inafanyika kwa nguvu kwa maelekezo ya wazazi tu.
Aidha alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa madaktari wa kufanya vipimo na kuchunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kuchunguza ubikra ambapo kazi hizo hufanywa na madaktari wanaume.
Kituo cha Mkono kwa Mkono kilifunguliwa miaka miwili iliyopita ambapo lengo lake kubwa ni kurahisisha kupatikana kwa huduma zote katika kituo kimoja za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo matukio ya ubakaji.
Kituo hicho kinachotoa huduma zake katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa kinatoa huduma zake kwa ushirikiano mkubwa wa mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na maendeleo ya mtoto na mwanamke ikiwemo UNFPA na UNICEF.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Kwishaaaa. Ukitaka bikra labda umzae wa kwako. Sku izi kitoto cha miaka kumi kilishapoteza bikra kitamboooo
ReplyDeletelkn znz ht bikra za tigo pia hazipo
ReplyDeleteHivi huu unyanyasaji mpaka lini! Bikira ni kwa mwanamke tu!? Unakuta jiyu zima linae kumuowa binti mdogo na lina taka bikira, wewe yako iko wapi??
ReplyDeleteMi napita 2.
ReplyDeleteWaweke na vipimo vya bikra za waname haki sawa kw wote,
ReplyDeleteDini
ReplyDeletebikra za zenji zimekimbilia bongo
ReplyDeletemaneno mengiiiii, nimeoa wake 2, na wote bikira
ReplyDelete