HELKOPTA YA CHADEMA YAPOTEA ANGANI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HELIKOPTA ya Chadema maarufu kama Chopa, juzi ilipotea angani na kusababisha viongozi wa chama hicho kushindwa kufanya mkutano katika Kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino, kama ilivyokuwa imepangwa kwenye ratiba.

Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imepangwa, viongozi wa kitaifa ambao ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (BAVICHA), walikuwa wafanye mkutano katika kijiji hicho saa 4 asubuhi.

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Steven Massawe alikiri kupotea kwa helikopta hiyo na kukanusha kwamba hakuna njama zozote zilizofanywa na CCM kutokana na kupotea kwa helikopta hiyo.

Kijiji cha Mpwayungu kipo katika Kata ya Mpwayungu, ambayo nafasi ya udiwani ipo wazi na vyama vya Chadema na CCM vyote vimesimamisha wagombea.

“Sababu kubwa ya kupotea kwa helikopta ni tatizo la mawasiliano kama mnavyojua Kijiji cha Mpwayungu hakina mawasiliano. Helikopta ilikuwa ifike katika Kijiji cha Mpwayungu saa nne asubuhi, lakini Kapteni alipotea na kusababisha kukaa angani kwa saa moja na dakika arobaini na akatua Kijiji cha Chipogolo.

“Alipofika Chipogolo akaambiwa sio kijiji hicho chenye mkutano na akatakiwa kurudi nyuma kwa upande wa magharibi kwa kilometa 40, hata hivyo hakufanikiwa ikabidi arudi mjini kujaza mafuta,” alisema Massawe.

Alisema baada ya kujaza mafuta, viongozi hao hawakwenda tena kufanya mkutano Mpwayungu badala yake wakaenda Mpwapwa ambapo kulikuwa na mkutano mwingine saa 7 mchana kwa mujibu wa ratiba.

“Leo (jana) hii viongozi hao kwa kutumia helikopta wamekwenda tena Mpwayungu na kufanikiwa kufanya mkutano majira ya saa nne asubuni na baada ya hapo waliekea Kijiji cha Segala Wilaya ya Chamwino, baadaye wataenda Kiteto na Moshi,” alisema.

Alisema sio kweli kwamba CCM walifanya njama helikopta ya Chadema ipotee ili isifanye mkutano katika kijiji hicho na kwamba Chadema na CCM vyote vilishafanya uzinduzi wa kapteni katika kata hiyo.

“Chadema ilifanya uzinduzi wake wa kampeni katika Kata ya Mwayungu, Januari 26 mwaka huu na CCM walifanya uzinduzi wao Januari 20,” alisema Massawe.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema iwapo Serikali ya CCM haitaweka mazingira ya haki kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kwa ajili ya amani ya kudumu, migogoro ya ardhi italitumbukiza taifa katika sintofahamu na hatari kubwa nchini.

Dk. Slaa aliyasema hayo kwenye mikutano ya M4C Pamoja Daima, jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Iselamagazi, Kishapu, Mhunze, Itilima, Lugulu na Bariadi.

Alisema ni haki kwa wananchi kuwa na matumaini, kwani ndiyo misingi wa amani ya kweli ambayo haihitaji kuhubiriwa jukwaani.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. http://internetduty.com/user/dashboard.php

    ReplyDelete
  2. We mnyika mashafu yamekutoka kwa pesa za wapiga kula wako! Cjui unaenda wapi na ndo mana mlipotea kwa umbeya wko Domo pana kwa kulopoka Ovyo, hivi unajua wananchi wa jimbo lako wanapata tabu ya Barabara? Unajua ungempigia waziri makelele yako hayo ungetusaidia sana kutwa kuwaambia Mawaziri wajiuzuru, ww umefanya nn jimbo mwako! Unashindwa kupiga makelele kila cku tutengenezewe barabara za,MBEZ via makongo juu & kutokes mbezi masana hospital? Au MBEZ via Maramba mawili situngekuona wa mana! , tungepunguza wote kujazana Ubungo Tafakali utaumia

    ReplyDelete
  3. Yaani 2015 sipotezi kura yangu tena kwa chadema jimbo la ubungo. Nawapa ccm najua watafanya wonders goba makongo, mbezi mwisho, hadi masana.

    ReplyDelete

Top Post Ad