JESHI LA POLISI LASAKA JAMBAZI LILILOUA WATU WANANE HUKO RORYA, TARIME

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndugu zangu waandishi wa habari, nimewaiteni hapa kwa dharura, ili kuweza kuwafahamisha hali halisi ya mauaji yaliyotokea katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya. Mnamo tarehe 26
Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada ya kukutana nao njiani. Siku hiyohiyo, majira
ya saa 4:00 usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo alimuua Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba na kumjeruhi mtu mwingine mmoja. Tarehe 27 Januari, 2014 majira ya 11:30 alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake aina ya Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19 ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu. 
Siku hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha Nkende. Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki
katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika kijiji cha Mogabiri.

Hadi sasa juhudi kubwa za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.  Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa
wananchi.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano ili jambazi huyo aweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka. Mwananchi mwenye taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba ya simu ifuatayo 0754 785557.

Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi,
 Kamishna Paul Chagonja
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. EE Mungu wangu tunusuru na watu kama hao,,,Mimi nafikiri hizi zama ndo zile za mwisho,,,Mbona mambo yanatisha sana jamani???

    ReplyDelete
    Replies
    1. NI KWELI KABISA USEMAVYO MDAU.HIZI NDO ZAMA ZA MWISHO.
      KWA SIKU MOJA TU MTU UNACHINJA BINADAMU WENZIWE KAMA WANYAMA!!!!,,SIKU YAKO IKIFIKA UTAMUELEZA NINI MUNGU WAKO?

      UDAKU SASA BLOG YAKO INASOMEKA VIZURI.YULE MSEMA MATUZI NA KUTUKANA WATU OVYO,UMEMUWEZA,UNADELETIA MBALI COMMENTS ZAKE ZA MATUSI......THANX

      Delete
  2. Ila inasemekana jambazi mwenyewe akili haziko sawa kutokana na matukio anayofanya anaua hovyo sana atachukua cm au pesa tu zamfukini ama asichukue kitu kabisa! ss jambaz gani atumie silaha kuiba cm nokia na ni kijijin mayb ni tochi.shida nikumkamata jambazi anamiliki silaha alafu ni chizi hahahaha.! poluc mjipange....

    ReplyDelete
  3. Polisi kazi kuvizia malori na kupokea rushwa pamoja na kukamata malaya barabarani jamani tuachane na hao malaya tufanye kazi kutafuta waalifu hao jambazi

    ReplyDelete
  4. 12:36 si walimkamata mamaako akiwa anajiuza!! manina zako

    ReplyDelete
  5. yaani wanamwinda jambazi mwenye bunduki na ngao !? !? !? tunaenda wapi watanzania???????

    ReplyDelete

Top Post Ad