JINSI MBWA 120 WALIVYOMTAFUNA MJOMBA WA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Walimvua nguo na kumtupa kwenye ngome ya Mbwa wenye njaa 120

.Rais Kim Jong Un alikataa mjomba wake kunyongwa bali kuliwa na mbwa akiwa uchi wa mnyama

.kiongozi huyo na viongozi wengine 300 walishuhudia ukatili huo wa kutisha

.Adhabu hiyo iitwayo ‘Quan jue’ ilidumu kwa saa moja

.Mjomba wake alishtakiwa kwa hila na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka

Na Damas Makangale, kwa Msaada wa Mtandao

Taarifa zilizovuja kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani ni kwamba Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un alishuhudia jinsi mjomba wake Jang Thaek akiliwa na mbwa karibu 120 akiwa uchi wa mnyama kama adhabu mbadala badala ya kunyongwa.

Taarifa zinasema kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliamuru mjomba wake avuliwe nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na kisha mbwa kumtafuna akiwa hai mpaka kifo chake, watetezi wa haki za binadamu wanasema ni adhabu ya kikatili ambayo dunia haijawahi kushuhudia kwa miongo kadhaa.

Watu wa karibu na wanafamilia wanasema Mjomba wake huyo alipelekwa kwenye ngome hiyo na wasaidizi wake watano na kuachiwa kwa mbwa wenye njaa ya siku tatu ili waweze kumshughulikia.

Maelezo ya kutisha yaliojitokeza katika ripoti katika gazeti la Straits Times la Singapore , ambayo lilisema kitendo hicho ni cha  kutisha na kinajulikana kama ‘ Quan jue ‘, au ‘ utekelezaji wa adhabu kwa kutumia mbwa wenye njaa.

Thaek , alivaa suti ya bluu na pingu akisindikizwa katika mahakama ya Desemba 12, aliuawa na mbwa mwitu , kulingana na ripoti kutoka China.

Taarifa zinaongeza kiongozi huyo wa Korea ya Kaskazini Kim Jong- Un alikuwa anatoa ujumbe katika sikukuu ya mwaka mpya kwa wakorea wote nchini humo.

Wachambuzi wanasema kiongozi huyo jeuri alikuwa na ujumbe maalum kwa viongozi walioalikwa kwenye sherehe ya kifo cha mjomba wake kama onyo kwamba wanapaswa kufuata taratibu na endapo kiongozi yeyote atakiuka taratibu adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. inabidi na sisi tuanze kuitumia hii adhabu!! kwa wala rushwa kama yeye!!

    ReplyDelete
  2. Bona hii poa sana tu, hasa lwa magamba walarushwa na mafisadi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tusisahau Wauza unga pia wanatakiwa washughulikiwe katika style hii.

      Delete
  3. siku moja watakiona cha mtema kuni, Mungu yupo, adhabu yao itakuwa hii (mafisadi, wauza sembe n.k)

    ReplyDelete
  4. Tanzania bado kidogo tuvute subira mpaka Madini na maliasili zingine ziishe

    ReplyDelete
  5. Jamani hata katika madini yote yanafundisha kusamehe sasa wewe ambaye umeshindwa kusamehe wengine je kweli wewe utatumainiya kama Mungu atakusamehe? Fikiria kwanza kama ni wewe kuliwa na umbwa mpaka kufa chukuwa ile maumivu iwe yako

    ReplyDelete
  6. dah! Wanatisha

    ReplyDelete
  7. Dih...eti oooooh na ss tuitumie hyo adhabu ili tukomeshe kula#mlungula..lhvi fikiria kama ndyo baba yako anapewa adhabu hyo mbele za raia na ww mwnyewe ukiwemo...!!

    ReplyDelete
  8. hv kweli malpo dunian

    ReplyDelete

Top Post Ad