ZITTO"DENI LA TAIFA WANAFAIDI WEZI WACHACHE LAKINI TUNALIPA WOTE"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Deni la Taifa: wafaidi wachache, twalipa wote.
Leo nimeandika kuhusu Deni la Taifa kukua kwa kasi na kufikia tshs 27 trilioni mpaka Desemba 2013 kutoka tshs 10 trilioni mwaka 2005. Baadhi ya Watalaamu wanajenga hoja kuwa kukopa sio shida, bali kukopa kwa ajili ya nini. Nikakumbuka mzigo wa madeni ambao Taifa lilibeba miaka ya sabini na themanini kiasi cha Tanzania kukoswa koswa kuwa nchi ya Kwanza duniani kushindwa kuhudumia madeni yake. ‘heshima’ hiyo ilikwenda kwa nchi ya Nicaragua mwaka 1982. Mikopo ya nini?
Mwishoni mwa miaka ya sabini Tanzania ilikopa dola za kimarekani milioni sitini (USD 60m) kwa ajili ya mradi wa Kiwanda cha viatu Morogoro. Lengo la kiwanda kiwanda kile ilikuwa ni kuuza viatu nchini Italia. Mwaka mmoja baada ya kiwanda kuzinduliwa kilikuwa na uwezo wa kuzalisha kwa ufanisi wa asilimia 4 tu ya uwezo wake na hakikuweza kuuza hata jozi moja ya kiatu nje ya nchi. Miaka ya tisini kiwanda kile kiliuzwa katika mpango wa ubinafsishaji na hivi sasa kimegeuzwa kuwa ghala. Hata hivyo Deni hili lilipwa na kila Mtanzania kupitia kodi.
Kesho Jumanne tarehe 28 Januari, 2014 Kamati ya Bunge ninayoongoza ya Hesabu za Serikali (PAC) inapokea taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa kuhusu Mfumo na Mchakato wa kusambaza pembejeo za ruzuku kwa wakulima. Ukaguzi huu umefanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG). Nimeipitia Taarifa hii na kukumbuka habari ya ‘Morogoro Shoe Factory’.
Bajeti ya pembejeo za ruzuku ya mwaka 2011/12 ilikuwa tshs 122.4 bilioni, kati ya hizo tshs 88.9 bilioni ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Taarifa ya CAG inaonyesha uvundo wa ufisadi katika mfumo mzima wa pembejeo za ruzuku. Katika kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa asilimia 70 ya wananchi waliorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia, hata hao waliopata mbolea walidai mbolea ilikuwa haina ubora stahili na matokeo yake uzalishaji wa mazao ulikuwa mdogo. Hata hivyo wasambaji wa mbolea walilipwa fedha zao zote. Afisa mmoja mwandamizi wa Benki ya Dunia alipata nukuliwa kusema kuwa asilimia 60 ya Bajeti ya pembejeo za ruzuku iliporwa na wajanja wachache. 
Deni hili nalo litalipwa na Watanzania wote japo waliofadika ni wezi wachache. Kinachosikitisha ni kwamba masuala haya yanayohusu wananchi hayapati msukumo kwenye mijadala ya kitaifa. Tusipobadilika tutajikuta tuna madeni mpaka kwenye kope za macho yetu. 
“...mikopo haisaidii, hata tukiitumia kujenga shule au hospitali au viwanda lazima ilipwe. Mlipaji ni mkulima wa vijijini...” Azimio la Arusha, 1967.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hilo nalo tunaomba mheshimiwa rais asilifumbie macho kwani nijanga la wananchi mtetezi wetu ni yeye tu tunaomba afuatiliye kama ya mafuriko ya moro

    ReplyDelete
  2. Well said Zittto, keep on informing us,gud job! People wat's a way forward?

    ReplyDelete
  3. Mpaka 2ingie msituni coz mmezidi mamb ya kisenge na lazima vita iume!

    ReplyDelete
  4. vita unaumwa nn au unajisemea 2 kisa mdomo hau2mii vocha, km huna point acha wa2 wazma watetee taifa co kuchochea vta km una ubavu wa kupambana.tafakr km mtanzania

    ReplyDelete
  5. Hilo senge hilo unafikiri vita ndo kuondoa tatizo kumamayo wewe..Angalia nchi zote zilizofanya hivyo Leo hii kiko wapi zaidi ya kuongeza matatizo..La muhimu kutafuta njia nzuri ya kutumia ili kuweza kuondoa tatizo...

    ReplyDelete
  6. hajui madhara ya vita....,tatizo hatuna mfumo wa kujenga taifa lenye ubunifu na uaminifu

    ReplyDelete

Top Post Ad