MASKINI TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI YAAMBULIA PATUPU TUZO ZA MOVIE AFRICA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watanzania tulifurahi kwa habari kuwa Tamthilia yetu ya Siri ya Mtungi imechaguliwa kuwania Tuzo Saba katika  tuzo za Africa Magic Movie Awards 2014’ Tuzo hizo zilifanyika jumamosi hii lakini kwa Bahati Mbaya Haikuweza kupata Tuzo hata Moja...

Kinachoumiza zaidi ni hata katika kipengele ambacho ilikuwa ni lazima Siri ya Mtungi ishinde cha Best Indigenous Language Movie/Series (Swahili) kilichukuliwa na Wakenya, Njoki Muhoho – Mama Duka.

Inatia wasiwasi kidogo kwakuwa hakuna fundi wa Kiswahili duniani kumzidi mswahili mwenyewe wa Tanzania. Inapofikia hadi Mkenya anachukua kile tunachokiweza zaidi, ni ishara kuwa tunahitaji kujitafakari tunakosea wapi. Ni kweli Wakenya ni mafundi wa Kiswahili kuliko sisi? Tatizo ni nini?

“Nadhani kilichopelekea Siri ya Mtungi kukosa tuzo ni vitu viwili, kwanza tabia ya Watanzania sisi kutopenda kupiga kura, hiyo ndio tatizo la kwanza, lakini pili crew ya Siri ya Mtungi yenyewe haikuwa na nguvu kubwa kwenye kushawishi wadau katika upigaji kura. All in all jamaa wako vizuri I hope next year tutafanya vizuri. Nadhani pia waandaaji wa Tuzo zozote Tanzania wamejifunza nini maana ya Tuzo,” anasema King David, mtangazaji wa Kings FM ya Njombe.

David yupo sahihi kwa mmoja. Ni kweli kabisa, lawama ije kwetu sisi wenyewe Watanzania tulioshindwa kuwa wazalendo kwa kuwapigia kura Siri ya Mtungi washinde, lakini mfumo wa tuzo hizo ulikuwa tofauti kidogo. Kulikuwa na jumla ya vipengele 27 na ni vipengele 9 tu kati ya hivyo ndivyo vilikuwa vya watazamaji kupiga kura na kuchagua mshindi.

Kwenye vipengele vilivyokuwa vikipigiwa kura (Votable Categories) Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa kwenye kipengele kimoja tu ambacho ni BEST ACTOR IN A DRAMA alichokuwa ametajwa ‘Juma Rajab Rashid’ aka Cheche.

Vipengele vingine 6 ambavyo Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa, vilikuwa ni vile ambavyo jopo la wataalam limekaa na kuchagua mshindi linayemuona ni bora katika kipengele husika. Mara nyingi katika mfumo wa aina hii, yote yanaweza kutokea na upendeleo na mapenzi ya nchi fulani fulani yanaweza kuchukua nafasi.

Kipengele cha kupigiwa kura alichokuwa ametajwa Cheche, kilikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Majid Michel ( Somewhere in Africa), Hlomla Dandala ( Contract), Majid Michel (House of Gold) na Tope Tedela (A Mile from Home). Ili Cheche ashinde, alitakiwa kupigiwa kura nyingi sana, na kwakweli haikuwa rahisi kuwazidi waigizaji wa Nigeria ama Afrika Kusini katika kipengele hiki japo yote yanawezekana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmh jamani hivi hizi movie za tanzania zinaishia bongo pekee?.mbona hazijitangazi nje kama kwenye magic afrika ?.hivi kweli wenzetu kenya wamechukua tunzo zaidi ya tatu sisi tanzania tupo wapi?.it mean tumeshindwa hata kuonyesha na sisi tunazo movie zinazopendeza ?.mbona zamani kidogo tanzania movie zinaonyeshwa kwenye magic afrika kulikoni?.zinatangazeni nje mtapata masoko na kuitangaza nchi yenu .msitutie aibu acheni porojofanyane kazi jitangazeni .

    ReplyDelete
  2. Lugha labda inachangia kuna wengine hawapendi kusoma subtitle. Sasa afadhali ya hawa subtitle yao ukija bongo movie uko ndo utajuuta mavitu ya ajabu ajabu. Wakiambiwa wakoseme hawataki wao wanalewa na umaarufu wa hapa hapa. Kufika watasahau unless wajirekebishe kuanzia saivi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mdau tusahau kusoma sanaa apo bagamoyo shughuli wanakudharau ilhali wanakuja wazungu kutoka nje kusomea. Pili wajifunze na lugha ya kingereza sio maneno matatu ya kuchupia chupia. Waige mifano kama wa kenya. Au basi wajipange vyema kwenye subtitle kama bollywood. Watafika!!

      Delete
  3. Mkiongelea tamthilia ionyeshwe atlist mara 3 or 4 kwa wiki,inaweza kuteka akili za watu naiwe na mtiririko mzuri na ichukue kwa uchache mwez na nusu.ss wabongo eti tamthilia inaonyweshwa mara 1 kwa wiki smtmz sehem zinarudiwa au haionyeshwi tu bila taarifa inatia uvivu kufatilia!afu wanaita tamthilia??? Kivp!? Baada ya mwez imeisha bwana eeee jipangeni kwa hilo bado sn! Hata hii siri ya mtungi haikua na mtiririko mzuri ninauhakika haikufatiliwa vzr na wengi ss nani ahamasike kupiga kura?leo hii ile tamthilia ya her mathers dghter ya star TV iwekwe ktk shindano hapa tu TZ nauhakika wengi wataipigia kura.so tatizo hatjui nn move??? Nn tamthilia. MJIPANGE!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni kweli hawaweki matangazo ya kutosha pia ili watu wajue inaangaliwa mda gani na lini ingewavutia wengi na wangeangalia na kupigia kura, kumbukeni kama tausi ya kenya watu walikuwa wanaacha kabisa kazi zao ili wasipitwe na tausi, au mambo hayo, kidedea lkn hiyo siri ya mtungi nakumbuka nimeioa mara moja sikuji sikujua tena imeishaia wapi lini na imeishaje

      Delete

Top Post Ad