MUME ATELEKEZA FAMILIA NA KWENDA KUISHI GESTI NA KIMADA..AFUMWA LIVE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Issa Mnally na Richard Bukos

HII ni ni fedheha! Mzee Mbonde, mkazi wa Kimara jijini Dar, anadaiwa kutelekeza familia na kwenda kuishi na mwanamke mwingine gesti kisha kufumwa laivu na mkewe, Herieth Mngodo.

Tukio hilo lililokusanya kadamnasi ya mjini, lilijiri wikiendi iliyopita katika gesti iitwayo New Samri, Manzese jijini Dar ikiwa ni sehemu ya kazi nyingine nzuri ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers.

SARAKASI ZA NDOA

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mzee Mbonde ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza- C, Dar, alidaiwa kuitelekeza familia yake (mke na watoto watatu) na kuishi na mwanamke mwingine katika gesti hiyo tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, Mzee Mbonde alioana na mkewe huyo mwaka 1984, bomani na ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja.
Kilidai, mwishoni mwa mwaka jana mzee huyo alianza, ‘kuchepuka kutoka njia kuu’ na kuanzisha uhusiano na mwanamke wa nje kisha kwenda kujichimbia naye kwenye gesti hiyo.

UMBEYA WAMFIKIA MKEWE

“Mjini watu watakunyima ugali siyo maneno, kuna watu walimtonya mama Herieth kuwa mumewe anaishi katika gesti hiyo ndipo alipovaa kininja na kwenda kufanya utafiti, akabaini kuwa ni kweli na kuwajuza OFM,” kilisema chanzo hicho.

OFM MZIGONI

Kikosi kazi cha OFM, baada ya kumegewa mchapo huo, kilitinga katika gesti hiyo na kupanga chumba ambacho kilikuwa kinatazamana na chumba cha diwani huyo mstaafu kwa siku tatu kuchunguza kama kweli kigogo huyo anaishi na mwanamke mwingine, ‘results’ zikaonesha ni kweli. 

MUVI LILIVYOANZA

Baada ya OFM kumpa majibu mke huyo wa diwani mstaafu, alikusanya nguo zote za mumewe akaambatana na mwanaye wa kike kwenda kwenye gesti hiyo kumkabidhi.

“Sitaki ugomvi na mume wangu, kaamua kunitelekeza na familia, dawa yake ni kumpelekea hizi nguo zake ili aendelee kuishi na huyo mwanamke wake hukohuko,” alisema mama huyo.

FUMANIZI KABANG!

Huku makamanda wa OFM wakifuatilia kwa karibu na kunasa picha hatua kwa hatua, walimshuhudia mama huyo akizama na Bajaj katika gesti hiyo, akagonga katika chumba cha mzee huyo, alipofungua tu, alimnyunyizia mumewe pilipili machoni na kuanza kumtupia nguo zake.

Timbwili zito liliibuka, mke alianza kumzaba makofi mumewe, ndani ya muda mfupi watu kibao wakajaa nje na ndani ya gesti hiyo kumshuhudia mzee huyo akiangua kilio, hali iliyowashtua wateja wengine waliopanga katika gesti hiyo.

MFUMANIWAJI ATOKA NDUKI

Wakati timbwili likiendelea, mwanamke aliyefumaniwa alifanikiwa kupata mwanya na kutokomea kusikojulikana hivyo msala ukabaki kwa diwani huyo mstaafu.

Mke huyo, baada ya kutekeleza matakwa yake (fumanizi), naye aliondoka eneo hilo na mwanaye kuelekea nyumbani kwao na kumuacha mumewe akiwa hoi kwa maumivu ya pilipili machoni kwani yalishaanza kuvimba.
GPL
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ushamdhalilisha unafikiri atarudi huyo

    ReplyDelete
  2. wanawake tupooooo iyo ndo dawa yao

    ReplyDelete
  3. sidhani kama kufanya hivyo ni dawa, tena kazaa nae hadi watoto, uyo mama kajizalilisha mwenyewe.

    ReplyDelete
  4. Utamu umeisha home ndo maana mzee katoka njia kuu

    ReplyDelete
  5. Utamu umeisha home ndo maana mzee katoka njia kuu

    ReplyDelete
  6. Akilo za kiafrika bana et mama kajilalilisha hilo libabu ndo halijazqlilika muwe mnafikiria kwa kutumia akili na sio mfumo dume matako mavi yenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. mmh ila kweli akili za kiafrica bwana ni za mfumo dume,libabu si ndo limedhalilika

      Delete
  7. Jaman utamuu!!!!!

    ReplyDelete
  8. Halafu hatajihita mwanaume, Mwanaume gani unakimbia nyumbani na kuacha watoto wako hata kama umpendi mkeo watoto je?watu wengine ni wanaume maumbile tu lakini si kiakili!

    ReplyDelete
  9. Kweli akili za kiafrika. Atadharilika mwenyewe. Kama jitu lishakuwa lihuni hata ufanye mambo gan kwa bed ni bure. Wanaume weng wa kiafrika hujifikiria wenyewe...

    ReplyDelete
  10. Huyo mwanamke pumbavu' kuna mafundisho gan ya kwenda kuchukua wambea wa hbr na kwenda kumwagia pilipili mumew? Tutajuaje kuwa mwanamke ndo aliemfukuza nymbn? Eti nampelekea nguo zake' asa kwa nn umwagie pilipil?ili iweje kwanza? Eti mwanamke aliekuwa nae alipata upenyo akakimbia,huenda cyo kwel'pengne alikuwa mwnyw..haiwezekan aende na wapiga picha kamera ikose hata picha moja ya mwanamke huyo aliekuwa nae' huyo mwanamke mshamba sana' namshaur mzee akirud nymbn 'piga chini atie adabu'najua anaishi kwny nymbn yako pumbavu kbsa.

    ReplyDelete

Top Post Ad