HII HAPA SIRI KWA WANAWAKE WASAKA NDOA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema..........hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu 
Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari 

Hii hapa > Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake: 
1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa. 
2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu". 

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!! 

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!! 

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana. 

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi. 

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Shukrani za dhati zimfikie mtungaji wa article hii ndg Masanja Mkandamizaji nawasilisha tujadili
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Upumbavu mtupu watu wanatumikishwa,wanafanyw mahouse gal na hawaolewi,ovyooooooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mdau, kama wa kuolewa utaolewa hata ucpofanya hayo, kuna mamburula kibao kutwa wanabandika kope hawajui hata kuchambua mchele na wameolewa, noma sana

      Delete
  2. unaweza kupika, kufua,kunyoosha, kumfanyia usafi ndani kwake, kumnunulia na vijizawadi na kibuti pia ukapigwa!!!!!!! inaumaje!! hayo mengine ni kujitutumua tuuuu!!!

    ReplyDelete
  3. Haya mambo ni ya msingi sana,kina dada kazi kwenu.

    ReplyDelete
  4. ndoa n zali tu ndg muandishi unaeza fua mpk fangas zmalize vdole lkn waaaap wanaume n mafala wasoridhika na hyo ya kumbania kum.a teh teh we unabana mwenzako anaachia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti ndoa Ni zali,wadada wanapenda kuolewa,sisi tulioolewa tunasali tuachike,

      Delete
  5. Hapana, kuwa tu, kama ulivyo, sasa u pretend una kea, na kujishughulisha nawakati si kawaida yako? Mmhh hapana just be who you are, kama ipo,ipo tu

    ReplyDelete
  6. Hawatabiriki Wanaume kwa sasa hata umfanyie nn

    ReplyDelete
  7. Kamawandoa niwandowa 2nakama nikiburudisho utazidikuwakiburudisho2

    ReplyDelete
  8. Mwanaume anaetumia vigezo hivyo ni dhahiri kua ni mkoloni haswaaa!

    ReplyDelete

Top Post Ad