INASEMEKANA DANCE WA DIAMOND AMEKAMATWA CHINA NA MADAWA YA KULEVYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

STAA  wa  muziki  wa  bongo  fleva  nchini, Abdul  Nassib  "Diamond"  ametakiwa  kutokanyaga  kabisa  nchini  China  na  kwamba  akitokeza  pua  yake  nchini  humo  asahau  kabisa  kurudi  uraiani...

Hiyo  inafuatia  kijana  mmoja  mtanzania  kukamatwa  wiki  iliyopita  uwanja  wa  ndege  wa   Macau   China  na  kudai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

Habari  kutoka  Macau  China  zinadai  kuwa  kijana  huyo  aliyejulikana  kwa  jina  moja  la  Manyota  alikamatwa  akiwa  kwenye  harakati  za  kuingiza   mzigo  huo  wa  dawa  za  kulevya  kwa  kupitia  uwanja  wa  ndege  wa  Macau....

Kwa  mujibu  wa  vyanzo  vyetu  vya  habari, inaarifiwa  kuwa  Manyota  alikamatwa  Alhamisi  ya  wiki  iliyopita  katika  uwanja  uleule  aliokamatwa  mtanzania  mwingine  Jackline  Patrick, anayesotea  rumande  mpaka  hii  leo  huko  huko  Macau  China.....

Kijana  mmoja  wa  kitanzania  anayefanya  shughuli  zake  huko  China  amedai  kuwa  Manyota  alikamatwa  na  maofisa  wa  usalama  wa  uwanja  wa  ndege  na  katika  utetezi  wake  alidai  kuwa  yeye  ni  mwanamuziki  toka  Afrika  Mashariki...

Mtanzania  huyo  aliendelea  kudai  kuwa, Manyota  baada  ya  kukamatwa  alianza  kubabaika  kwa  kujifanya  mwanamuziki  na  baadae  akadai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

"Alijifanya  yeye  ni  mwanamuziki, baadae  akabadilika  na  kudai  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania  na  kwamba  ndani  ya  ule  mzigo  alikuwa  hajui  kuna nini  zaidi  ya  kuombwa  na  jamaa  zake  wa  Dar  awapelekee  nchini  China"...Alisema  mtanzania  huyo

Inasemekana  kuwa, ili  kujiridhisha, maofisa  hao  wa  usalama  wa  uwanja wa  ndege    walimtaka  kijana  huyo  aoneshe  moja  ya  kazi  zake  na  yeye  akaishia  kuwaonesha  moja  ya  video  za  Diamond  kupitia  mtandaoni  na  kumuonesha  mmoja  wa  wacheza  shoo  wa  mwanamuziki  huyo  kuwa  ndo  yeye  Manyota...

Inasemekana  kuwa, pamoja  na  utetezi  wake  huo  ambao  unaweza  kumuingiza  matatani  Diamond,maofisa  hao  wa  usalama  walishndwa  kumuelewa  na  kumtupa  ndani.....

Mtanzania  huyo  alihitimisha  kwa  kudai  kuwa, kutokana  na  mazingira  yalivyo,ni  vyema  mwanamuzi  Diamond  akawa  makini   sana  kama  atakuwa  na  safari  za  kwenda  China  kwani  kwa  namna  moja  ama  nyingine  jina  lake  limewekwa  kwenye  orodha  ya  majina  machafu   na  wanaweza  kumkamata  kwa  lengo  la  kuujua  ukweli....
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tobaaa makubwa, haya, itajulikana tu ngoja tuone, utajiri bongo bila madawa hauwezekani

    ReplyDelete
  2. Hiyo scandal lazima diamond ajuwa hayo.wote wamoja nibogi hilo limetumwa.

    ReplyDelete
  3. duh ni shidaaaaaaaaa utajiri wa bongo ngoja tuone mwisho wake

    ReplyDelete
  4. Mamaaaaaaaaaaa!asalaleeeee,utajiri bongo Ni u freemason au sembe basiiiiiii

    ReplyDelete
  5. pelekeni huko! kwendeni zenu wapuuz nini nyie hv mnamtaka nn mtoto wa watu? hv mpka mmtoe uhai wake ndo mfurah ee? kila siku kumxema mtoto wa watu hv hamchoki? au mnadhan anamyo wa chuma ee? ushamb huo mtoto wa wat anahangaik kila ck af leo mnakuja kuja 2 hap kuleta habr zisizo na kichwa wala mguu mtamuua mtt wa watu kha! roho mbaya zmewakaa! cjui mpoji

    ReplyDelete

Top Post Ad