Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.
“Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa vizuri ile mbaya.
“Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga safari hii basi tena,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni Chako.
Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: “Unajua hii biashara inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao kabisa.”
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.
Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.
Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.
WAO WASEME BIASHARA IMEKUBARI,HAPO NI FULL KUAMBIKIZWA,WAKIANZA KUHARISHA WATASEMA WAO WENYEWE.
ReplyDeleteSiwanawalipa navirusi kabisa itafahamika tu likianza degedege la ukubwani
ReplyDeleteaaaaah jamani mnanichekesha......na vimewajaa hao wabunge na wazairi balaa!!!!!
DeleteWabunge awatumiiga condom why?
DeleteSpeaking from experience au?
Deleteilo kuma halijielew apo juu yako
DeleteNi wao na mungu wao ngoja waambukizwe
ReplyDelete