MCHUNGAJI MTIKILA ADAI AMEZUIWA KUCHANGIA BUNGENI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila amedai hataweza kuchangia tena katika mjadala wa Katiba kwa kuwa Ofisi ya Bunge imempiga marufuku kutokana na kauli zake.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad alisema kuwa taarifa hiyo kwake ni mpya na haamini kuwa jambo hilo lipo.

“Hili kwangu ni jipya na sidhani kuwa linawezekana na lipo,” alisema Hamad.

Awali Mtikila aliliambia gazeti hili kuwa amepewa barua hiyo Jumatano iliyopita, ikiwa ni majibu ya barua yake aliyoandikia ofisi hiyo ya Bunge kutaka ufafanuzi wa kile alichoeleza kuwa amekuwa akinyimwa haki ya kuchangia bungeni.

“Nilianza kuhisi baada ya kuona kuwa nanyimwa kuchangia, nikaandika barua kuomba maelezo kwa nini ninakosa nafasi ya kuchangia bungeni,” alisema Mtikila na kuongeza;

“Lakini juzi nilipokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge ikinikataza kuchangia tena bungeni kutokana na statement (taarifa) zangu za kukosewa kwa mchakato.”

Alisema kuwa alipomuuliza katibu kulikoni akatazwe kuchangia katika Bunge hilo alijibiwa kuwa ni maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta.

Mchungaji Mtikila alisema kutokana na katazo hilo atamwona Sitta ili amfafanulie tatizo lake.

“Hii imeniathiri sana mimi. Bunge hili limepotoka wanachoangalia ni masilahi yao na si ya nchi,” alisema.

Alisema mchakato wote umekosewa kwa kuwaweka wabunge na wawakilishi kuwa sehemu ya Bunge badala ya wananchi kuchagua wajumbe wa Bunge hilo.

“Hakuna nchi yoyote ambayo imefanya hivyo, wanaharibu mabilioni ya fedha ambayo hayataleta Katiba yenye uhalali yoyote,” alisema.

Alisema endapo Sitta atashindwa kutatua jambo hilo anakusudia kuunganisha katika ushahidi wake kwenye kesi inayopinga mchakato wa Katiba.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mzee anambwembwe sana, ila anachoongea hapo ni sawa kabisa

    ReplyDelete
  2. Anataka umarufu

    ReplyDelete
  3. kazuiwa na nani huyu baba kwa atention hajambo, ulishikwa mdomo kuongea wewe shwain

    ReplyDelete
  4. baba mtikila shikamooo mze wetu chukua tu urais utozuiwa na paka yeyote shwain weweee,

    ReplyDelete
  5. wewe mze ukapimwe ubongo sindio ww ulisemaga baba wa taifa mzee kifimbo kafa kwa ukimwi?

    ReplyDelete
  6. Ana laana huyu mzee

    ReplyDelete
  7. Acheni Matusi mzee wetu sisi watanganyika.Huyu mtu anaona mbali sana na ana uwezo mkubwa wa akili zaidi yenu na wazazi wenu.Na uwezo huo ndio umempa heshima aliyonayo.Kuhusu Mwalimu Mkapa mwenyewe alisema alikuwa upungufu wa kinga mwilini

    ReplyDelete
  8. Hana lolote anapenda sifa dana na kesi. Rais alikuthini na kukureshimu kukupitisha ila hujui thamani. Acha sifa umeshazeeka mambo ya kedi achana naye

    ReplyDelete
  9. pole mzee wangu tumianjia nyingine kutafuta umaarufu hapo umebuma

    ReplyDelete
  10. Hivi DINI na Siasa wapi na wapi?mi siku hizi siendi kanisani,hawa walokole ni biashara tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad