MLIPUKO WA MABOMU TENA KENYA...SITA WAFARIKI DUNIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa  na washambulizi waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jaman kenya kuna nn? Mbona amani inatoweka taratibu kila kukicha, polen sana nchi ya kenya, R.I.P

    ReplyDelete
  2. RAIS KENYATTA WAFUKUZE WAKIMBIZI WOTE WAENDE KWAO,NDO CHANZO CHA KUKOSEKANA AMANI NCHINI KENYA.

    ReplyDelete
  3. Hawa wasomali bora warudishwe kwao kwa nguvu sasa kenya yetu nzuri amani hakuna tena si nairobi si mombasa huu ugaidi umezidi.Hasa ni kitu gani kinawasumbua ama wanakitaka toka serikalin?sasa wakiua raia wa kawaida ndo nini?jamani uhuru do somethng nchi yetu itashuka kiuchumi na tutakuwa wa kimbizi mambo haya yakiendelea.na warudi kwao wakaendelee kuuana wao kwa wao mana wamezoea ila watuwachie nchi yetu kwa amani.Kipindi hiki ndo namkumbuka idd amin wa uganda mbona wangekuwa wameregeshwa kwao zamani.

    ReplyDelete

Top Post Ad