NGASSA AIPA YANGA BALAA LA KUKOSA UBINGWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSIMU uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga walikuwa mabingwa watetezi na walitumia zaidi ya Sh250 kuwasajili wachezaji watatu ambao ni kipa Juma Kaseja aliyevuna Sh40 milioni, Mrisho Ngassa aliyechota Sh30 mil na mshambuliaji Emanuel Okwi aliyeigharimu Sh180, mil.

Lakini imekumbana na balaa la aina yake imeshindwa kutetea ubingwa wake na kufanya winga wake machachari ambaye ni Ngassa kuandika rekodi ya mkosi kwa kupishana na ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa miaka mitano mfululizo.

Iko hivi; Ngassa alijiunga na Azam FC Juni 2010 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga ambayo kwa msimu huo uliomalizika haikunyakua ubingwa wa ligi. Simba walitwaa ubingwa wa msimu wa 2009/2010 tena kwa rekodi ya kutopoteza mchezo.

Mchezaji huyo aliichezea Azam kwenye msimu wa 2010/2011 na kuibuka mfungaji bora wa ligi akifunga mabao 18.

Lakini Azam ambayo ilikuwa haijawa tajiri kama ilivyo sasa, haikufanikiwa kutwaa ubingwa kwani ilimaliza nafasi ya tatu na pointi zake 44, huku Yanga wakiibuka mabingwa wa msimu huo.

Ngassa aliendelea kukipiga na Azam kwenye mwaka wake wa pili wa mkataba msimu wa 2011/2012 na licha ya kiwango chake kuwa juu kwenye msimu huo, timu yake iliambulia patupu ikimaliza ya pili katika ligi na Simba ikawa bingwa.

Bahati ilizidi kuwa mbaya kwa Ngassa baada ya kuuzwa na Azam kwenda Simba msimu wa 2012/2013 ambako nako alishindwa kuwasaidia Wekundu hao na kujikuta wakishika nafasi ya tatu huku Yanga ikiwa bingwa.

Nuksi ikaendelea katika msimu uliomalizika hivi karibuni ambapo alijiunga na Yanga, amepishana tena na ubingwa kwani sasa umeenda Azam. Ngassa amemaliza msimu akiwa na mabao 13 huku Yanga ikiwa imemaliza ya pili na pointi 56 huku Azam ikitwaa taji kwa pointi zake 62.

Mbeya City imemaliza ya tatu ikiwa na pointi 49 na Simba ya nne pointi 38.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad