WEMA AMFUNGIA DIAMOND, ASHINDWA KUMZIKA MZEE GURUMO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
HAYA yanaweza kuwa ni mambo ya malovee! Kuna madai kwamba Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ alishindwa kushiriki zoezi la kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo ‘Maalim Gurumo’ kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake madam Wema Sepetu, Ijumaa linakudadavulia.

Imedaiwa kuwa, Wema alimfanyia ‘umafia’ mpenzi wake huyo, Aprili 15, mwaka huu ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa marehemu huyo kuagwa nyumbani kwake Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki, Kisarawe, Pwani.

Itakumbukwa kuwa, Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni kama amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.

“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa gari Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.

Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo, walibaini kuwa, Diamond hakutia ‘maguu’ hivyo shughuli ya kumsaka ikaanza.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.

Mapaparazi hawakuchoka, wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa mwanandani wake Wema, Makumbusho, Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa, Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.


Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia waliambiwa wapendanao hao bado wamejifungia ndani, wakaondoka hadi muda wa jioni baada ya shughuli za mazishi, walirejea na kuambiwa Diamond alitoka muda si mrefu pasipo kujulikana alikoelekea.

Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda  mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.

“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena tumefika muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi amini tulijumuika kuupandisha mwili kwenye gari na sisi tukarudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu,” alisema Babu Tale.

Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.

“Mh! Nilikuwepo msibani ila sikwenda kuzika tu maana nilikuwa na Babu Tale pale na tulikuwa karibu kabisa na gari la Global Publishers, mara tu baada ya kumaliza kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari tuliondoka na kurejea kwenye majukumu yetu,” alisema Diamond.

Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwa nini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!
GPL


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Diamond anajua kitu kilimzuia asiende msibani hiyo story ya Wema ni cover up sio kweli

    ReplyDelete
  2. Yeye ndio amemu uwa ndo kwamana akuwepo

    ReplyDelete
  3. Mbona mnapenda sana kufatilia maisha ya watu mbona akiwa anakunya hamtuambii achen hizo ana maisha yake d nilikuwa nae mm msimseme wema

    ReplyDelete
  4. alifanya vema kumpa zawadi yake kabla ya kifo , binafsi sipendi michango baada ya kufa

    ReplyDelete

Top Post Ad