Hii Ndiyo Miaka Waliyomuongezea Arsenal Kocha wao Kwenye Mkataba Mpya.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha wa Arenal Arsene Wenger leo ametia saini mkataba wa miaka miwili kama meneja wa klabu hiyo hadi mwaka 2017 Wenger ambae kwa sasa ana miaka 64 ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996.
Msimu huu Wenger ameongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu la mabingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka 9 dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe la FA Cup.
Mkataba wa Wenger ulikua unamalizika mwaka huu ingawa Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.
Wenger ambaye kwa sasa ni meneja mkongwe zaidi katika ligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu mwezi Mei mwaka 2013,anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza.
Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Premier kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.
Wenger pia alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.

Hii ndiyo rekodi aliyoiweka Arsenal Wenger.
Ligi ya Premier:1998, 2002, 2004
Kombe la FA:1998, 2002, 2003, 2005, 2014
Kombe la Community Shield:1998, 1999, 2002, 2004
Kombe ya ligi ya klabu bingwa nafasi ya 2: 2006
Nafasi ya pili kombe la Uefa Cup:2000
Nafasi ya pili Kombe la League:2007, 2011
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wenger tumekuchoka, icho ki cup cha FA kickupe kibuli.... Yan ungekua bongo kabila lako mpare

    ReplyDelete

Top Post Ad