Mastaa Kumfungia Kazi Mpoki kwa Udhalilishaji Siku ya Kill Awards

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIMENUKA! Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa mwanasheria wao, Ijumaa Wikienda lina ishu nzima. 
Mujuni Silvery 'Mpoki'.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’. 
Aisha Mashauzi.
Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny Love. WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata nafasi ya kujitetea (balansi). 
Asha Baraka.
“Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama mnavyofanya magazetini. “Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si mwingine,” kilisema chanzo hicho. Maimartha wa Jesse. MADAI YAO YA MSINGI
Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao- kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki. KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka. MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano. RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans. 
Wema.
KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi! VANESSA; alimwambia afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si vyema kuyaandika hapa).
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

38 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mpoki kuwa Mc alisomea wapi huwezi kumuarika sehemu ya heshima kila mtu anataka kuheshimiwa aomba msamaha na abadilike

    ReplyDelete
  2. safi sana mpoki wachunie tu hawawezi kukufanya chochote

    ReplyDelete
  3. Waombe msamaha kwan ni utan tu.

    ReplyDelete
  4. Wape wape x10. c wao wanataka wasfiwe tuhu! n mekukubal. cku nyingine do da same bro.

    ReplyDelete
  5. Hana lolote ajasoma huyo kwa mc msomi asingekuwa na usubutu wa kusema mambo binafsi ya watu pia alikuwa anachaguwa watu wa kuwashushuwa mbona akumpa makavu Ray C? ni punguani wa akili huyo mpoki jeusi kama mkaa

    ReplyDelete
  6. KAWAIDA BWANA ME CKUONA ALIPOKOSEA COZ ALIKUA ANAWATANIA WOTE JAPO WABONGO UKIWATANIA KWENYE UKWELI WANANUNA ALIFANYA POA TU AISEE HAKUNA KIBAYA

    ReplyDelete
  7. muacheni mpoki wa watu kwani uongo.!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Omba Msamaha Mpoki Kwan Ni Utan 2.

    ReplyDelete
  9. wote hao Mirembe day (vichaa), namshukuru mpoki kutujulisha maana bila kuwatania tusingejua

    ReplyDelete
    Replies
    1. kasoro wema..alafu watu wote hapo wamshitaki mtu mmoja ka wasenge baridi awana jipya huyo asha baraka sura kama goti..wanakome..na hamna kesi.

      Delete
  10. hzo ni dhalau huwezi kuzalilisha mtu mbele ya umati mkubwa kiasi hcho, mfano mzuri ni pale wema alipokuwa akimwita mpenzi wake dimnd kuwa ni baby, yeye hakupaswa kumdhalilisha wema kiasi kile, kwani ndani ya ula ujumbi kuna ambao wanampenda na wasio mpenda, hvyo aliwapa nafasi maadui zake kuongeza bidii ya kumzomea, kwakuwa walipata sapoti kutoka kwa mpoki, akamatwe, na shelia ichukue mkondo wake. mpaka wageni wa nchi kutoka nchi mbalimbali walikuwa wakishangazwa na ktendo cha mpoki, hafai kupewa nafasi yoyote tena ya umc, kazi ni kudhalilisha watu. yakwake au ya mpenzi wake mbona alikuwa hasemi. na yule mtangazaji mwenzie wa kike alidhalilishwa sana, wadada msukae kimya juu ya hli. anafkili wote walikuwa wanafulahishwa na ule upumbafu wake cyo. ashikishwe adabu.

    ReplyDelete
  11. wapewapeeee vidonge vyao wakimeza wakitema shauri yao.sema mpoki wamezid kwan kwenye magazet na live zote si taarifa.wasikukoseshe usingiz bg up.wanapenda sana kusifiwa.afadhal uliwachana.nitakupa kazi yangu unafaa

    ReplyDelete
  12. Rais mwenyewe huchorwa kama katuni kulingana na matukio na nyakati tofauti tofauti...... mpoki was and still is so damn right dudes! Hata kwenye maharusi ma mc huongelea hukusu sifa (nzuri na/au mbaya) za makabila ya maharusi japo tz hatuna mambo ya ukabila ila pale huwa hakujengwi chuki zozote na huwa watu wanasifu kwa ushereheshaji ule.... Mpoki waache wakuite mahakamani bure nitakusimamia na tutashinda!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bongo ma superstar wapuuzi wanaojifanya wamejanjaruka ni wengi ila mmmppphhhh upuuzi mtupu..... ndio maana wengine walitaka kumgomea Diaomond kwa kuimba mbagala.... mtu mzima yuuuuleee anapeta wanaisoma number!

      Delete
    2. hata wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu waliambiwa wanavuta bangi.... je walikuwa wamekatwa nazo??? Yes Mpoki was so right!

      Delete
  13. Daaaaah wabongo. shame on you mnaotaka kumpeleka kwa Pilato Mpoki. take a time na jaribu kumwangalia Chriss Rocky wanataniwa maraisi nn masupastaa uchwara

    ReplyDelete
  14. wema mke wangu

    ReplyDelete
  15. Mbona huyu mpoki anafanana na kiongozi wa boko haramu sn? jamani huyu Abubakari shekau ni ndugu na mpoki jamani sura nzito na madevu hivyo hivyo kuna wanaume wenye asura nzito hao wawili wamezidi khaaa

    ReplyDelete
  16. ni kweli mdau copy kabisa uwezi jua pengine kakake na huo weusi na madevu aisaidie serekali ya naija walipo hao mateka aiseeee umeonaeee na ww ipate hiyo utani unaoendana na ukweli

    ReplyDelete
  17. Mi naona Mpoki alifanya vizuri sana! Aliwafanyia comed ya live, wamezoea comed za uongo? Mi nakupa hongera sana mpoki, niliipenda sana ile staili yako.

    ReplyDelete
  18. Mwacheni mpoki wawatu yale ule ulikuwa utani kama kupeleka mtu mahakamani angempeleka Elvis mbona amerushiwa ndizi ameila je? Mngeweza kama elvis huo utani amesha chorwa sana mkapa mbona hajapagawa acheni mambo yenu mlitaka msifiwe sasa amewaponda kudadadeki

    ReplyDelete
  19. Wabongo bado sn

    ReplyDelete
  20. mpok komed kama komed kama mtu anakili timamu hawez kufanya kitu km hicho wabongo bado sanaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  21. Mpoki nakupenda bure wabongo wengi ni mambulula awataki kuambiwa ukweli na inabidi uendelee kuwapiga madongo hivohivo wala wasikutishe mpoki up juu shikamoo mpoki.

    ReplyDelete
  22. Kaza buti Mpoki, hizo ni kelele za mpangaji. Usirudi nyuma

    ReplyDelete
  23. WOTE MNAOLALAMIKA HAMUELEWI MAANA YA COMEDY. NDIYO MAANA ANAIGIZA COMEDY. PALE ALIKUWA KAZINI. NA KAZI YAKE NI NINI? MASTAA KUWENI WAELEWA. KAZI YAKE NI .........

    ReplyDelete
  24. lakini mkumbuke kuwa pale haikuwa sehemu ya kufanya comedy, ni sehemu ya kutolewa tuzo! ingekuwa ze comedy show live! kweli lakini vitu viwili tofauti, kiufupi awaombe radhi, pia utani una mawili kukubali au kukataaa sasa wao wameukataa, na vile vile Kitanzania utani ni wa ukabila na kabila na sio masupa staa kwa comedian

    ReplyDelete
  25. http://cashnjob.com/index.php?refer=109808

    ReplyDelete
  26. ETI ASISEME???
    ......NANI KASEMA!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  27. ukweli unaumaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  28. ila kapitiliza alipendez lkn katania ila utani wa kweli halafu na si sehemu yake pale, watu walikuwa atention kupokea tuzo yeye anawaponda ila si ustaarabu

    ReplyDelete
  29. Mpoki njoo huku nigeria ujiunge na boko haramu,

    ReplyDelete
  30. Mbona mmelishikia bango hivi wakuda nyie?kwani lipi la kudhalilisha alilosema mpoki?ukweli mtupu na siku zote ukweli unauma.tupo tuliovunjika mbavu.eti sio mahali pake,kwani comedy kwake ni wapi?mmepashwa mpashike,Mpoki omba msahama bora liende lakini sio eti sheria itakushinda,wametaniwa wakina pinda,jk,komba nyie akina nani!mkome.

    ReplyDelete
  31. Nimekupenda mdau 7.28

    ReplyDelete
  32. Mpoki usijarishe sana ni kelele Tu za kware hao hawana mapya and tell Dem to hell

    ReplyDelete
  33. hahahahahahahhaaaaaaaa mpoki nazidi kukupenda.

    ReplyDelete

Top Post Ad