Flora Mbasha Avamiwa na Watu Wasiojulikana, Polisi Wamuokoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine yameibuka.

Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.

Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa  saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.

“Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango,” kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.

Alizungumza na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: “Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.”

Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye aliingia kwenye  gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.
GPL
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

29 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizo nimbinu tuuu za mrs mbasha kutaka kurudi kwa gwajimas wake Hana lolote hotel in pamemunogea hakuma cha kuvamiwa wala nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona Heeeeee Flora umeshamuua mumeo Mbasha kiroho,sasa unataka ummalize kimwili?Malaya we ebu mwache Mbasha Wa watu we endelea na gwamaji wako,uongoooooo mtupu bazazi weeee

      Delete
  2. Flora umetuchosha na ujinga wako ww mlokole gani jaman mbona huishi vitimbwi acha uongo mwanamke heeeeee tumekuchoka

    ReplyDelete
  3. Hivi hii Habari inatusaidia nini,mbona ujinga ujinga tu.

    ReplyDelete
  4. Liongooooo kweli hili limalaya,akuna cha kubamiwa wala nini kanogewa kukaa hotelini,kisaaaa gwamaji.Hivi mnatupa picha gani tunaosali makanisa yenu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wajinga! Sali na muombe Mungu wsko nyumbani.

      Delete
  5. flora ni shetan

    ReplyDelete
  6. Mwache Mbasha akae mafichoni Kama Ni kweli,makomandooo hayo 30,ya hapo kanisani kwa ha...la yako yanaweza mmaliza vilevile

    ReplyDelete
  7. Cheki picha hapo juuu anavyotunga uongo,picha inakionyesha

    ReplyDelete
  8. Hata Kama Mbasha kabaka ulitaka abake mbuzi?umemkimbia mumeo kitambooo ukaenda kupangishiwa hotelini mdogo wako na mipaja Yake minene kutwaaaa kuvaa vimini na kumtega Mbasha wewe uko ukoooo unatumbua tunda lililokatazwa.nyoooooo

    ReplyDelete
  9. Huyu dada muongooooooooo alimbambikiaga gonjwa la ukimwi mchumba wake Wa kwanza,akakimbilia kwa Mbasha,kumbe mchumba wake walaaaa hakuwa na ukimwi,kaka Wa watu aliliaaaaa ka mtoto,How could you?flora?shentwain weee

    ReplyDelete
  10. Mh miananiboa kweli huyu florah.hanamaana ulokole wake wakuigizia movie

    ReplyDelete
  11. Hii ni Ze comedy au comedy origino?

    ReplyDelete
  12. Uwongo hautakufikisha kokote FROLA....embu muogope mungu wako we mjaa laana.....so muendelee tu kula Bata na hyo bwanako..mwachen mtoto wa watu apumue...usifanye ajute siku alipokutana na we....dunia ya as si km ya zaman kuwa MTU unaeza mdanganya kirahis hivo nyau ww

    ReplyDelete
  13. Frola Mbasha akiwa kichwa wazi amkwisha lichafua kanisa na Wachungaji, pichani anaonekana anakuja na ushungi misikiti na Mashehe chungeni huyo jini mahaba asije hamia kwenu kuwachafua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwikwiiiiii mdau umeuaaaaa!mbavu zangu mieee

      Delete
  14. Frola mrudie Mungu kwakweli hivi vitimbi vyako tumekuchoka,acha kumtesa mumeo na uongo wako kama unaona Gwajima anakufaa basi hamia kabisa huko muache kijana wa watu apumue.Mungu akusaidie upate kuitambua kweli ili uwe huru.

    ReplyDelete
  15. jaman heb tuangalie mathara ya yale tunayofanya leo mnawapoteza kondoo kwa kutokuw makin hiv nyinyi hayo mambo c ya ndan ya ndoa kwanini msiyamalize huko kuliko kutufaidisha cc watu wengine ambao hayatuhusu.kila ndoa inamatatiz yake lakin hakun anae tangaza ni ww tu florah jipange dada Mungu akusaidie nimejikuta kukuchukia

    ReplyDelete
  16. pole flora wamezoea kuonea wanawake sasa abake mwingine matusi utuakanwe ulobakiwa pole wanawake hatutaonewa tena.walitaka ulie kimyakimya ampe na mimba kabisa.

    ReplyDelete
  17. huyu dada kakataa katakata, kuendelea na ndoa kabembelezwa masaa 6 anajibu shoti and clear sitaki ndoa nataka nimfunge, habari za ndani zinadai. eti anataka milioni 60 na kesi hafuti. kweli Emmanuel kaonewa sana mkaka wa watu mzuri. Mungu ndio atakaejibu

    ReplyDelete
  18. angekuwa ana mjengo mbezi beach na magari au sehemu yoyote angekuwa na jeuri ya kumwacha mume wake, sasa hana kitu anakaa hotel uchwara za sinza, Mungu anataka kilammoja amsamehe mwenzie. Yesu alikufa kwa ajili ya waovu wote pamoja na pia alimsamehe mwanamke aliefumaniwa, sembuse yeye. mxiuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  19. kaupatia umaarufu kupitia mume wake, unajua hata kama mumeo ni jambazi kakamatwa unatakiwa uwe upande wake. baadae utamuonya atabadilika, sio uungane na wanaomshitaki. kweli watu wengi hawajui maana ya mke mwema,. sio kupiga goti, wala kumsalimia vizuri wala kumpikia tu. bali akiwa kapata matatizo yoyote yale inatakiwa mwanamke mwema kutkumgeuka

    ReplyDelete
    Replies
    1. seriously!!!!kiapo kwa shida na raha sio dhambi na utakatifu. Hata mbingunk kila mtu ataubeba mzigo wake.umeua huko mke akutetee lol.hata MUNGU apendi.

      Delete
  20. Sio siri usilitukanishe jina la Bwana, ni aibu unayo fanya tangu lini ndoa ya kikristo ikavunjwa, unamweka mumeo kwenye wakati mgumu na kumtamani mke wake. Mtu kama kakosea hata kama ni kweli ukikataa kumsamehe mwenzako hata kanisani usiende utakuwa unapoteza muda wako na sadaka zako NA UNAKUWA CHUKIZO MBELE ZA MUNGU. Asiporudiana na mumewe mimi hata CD, wala Tamasha lolote la kwake kama akiweza kulifanya maana sidhani kama wakristo watakukubali tena Sisikilizi wala siendi.

    ReplyDelete
  21. Utasemaje unampenda Mungu usiyemwona, na wakati jirani yako( mume) unamchukia au humsamehe hata kama ni kweli. ukisamehe utakuwa queen of Gospel usiposamehe, utahudhuria kesi kwenye mabenchi ya mahakamani na Mbasha hatafungwa na itakuwa aibu kwenu na familia. wenye akili wote wameelewa mchezo unaofanyika. Maana kumbuka mawazo yako juu ya Mbasha sio sawa na Mawazo ya Mungu juu ya Mbasha. Mungu anamwazia meme kumpa Tumaini siku zake za mwisho. Sasa mpango wako wa kumfunga kama unafanana na wa Mungu Mbasha atakaa nyuma ya nondo za segerea. kama sio Mungu atakuwa kinyume na wao watendao kwa kiburi utaaibika na Mbasha atainuliwa na utamkuta kwenye siti ya Mbele Mbinguni. Kumbuka lile neno la Mungu malaya watawatangulia kuingia mbinguni. USIJIDANGANYE BI SHOSTI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. story hii ingekuja kwa design ya mbakwaji kulalamika akieleza madhara yalompata bila kumtaja muhusika no nyie nyie mngesema serikali imtafute mtuhumiwa sijui nini nini leo mnasema asamehe!!!!!!wapendwa sheria msumeno inakata kulia na kushoto.MUNGU anasemehe but msizani huwa hatoi adhabu.

      Delete
  22. Flora muongo sana kama hajaokoka jamani

    ReplyDelete
  23. Milokole tupa kuleeeer

    ReplyDelete
  24. Mda wote ulokuwa unafanya uzinzi hotelin.leo mungu anawafichua unasema majaribu

    ReplyDelete

Top Post Ad