Mhadhiri UDSM Ndio Rais Mpya wa Malawi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa ushindi wa Profesa Mutharika katika kiti cha urais wa Malawi, anaongeza idadi ya jamii ya wasomi waliopitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ama wakiwa wahadhiri au wanafunzi, kwani alifundisha chuoni hapo mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Nje ya kazi za uhadhiri, Profesa Mutharika aliyebobea katika masuala ya sheria ambaye pia ni mwanasiasa mzoefu na mashuhuri, ameshika nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, nafasi aliyoishika hadi anaingia katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.

Mbali ya Profesa Mutharika, wasomi wengine waliopitia UDSM na kufanikiwa katika ulingo wa kisiasa na hata kuwa marais au viongozi waandamizi katika nchi zao ni Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa zamani wa Zaire (sasa DRC) Laurent Desire-Kabila.

Aidha, Makamu wa Rais wa zamani wa Uganda, Eriya Kategaya alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama ilivyo kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan, John Garang.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba, naye alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama ilivyo kwa Mawaziri wakuu watatu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.

Getrude Mongella, Rais wa zamani wa Bunge la Afrika ambaye pia alishika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa sasa wa Tanzania,naye amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Watu wengine mashuhuri waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni pamoja na mwanasheria Mkuu wa Kenya, Dk Willy Mutunga na Donald Kaberuka, Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambaye ni raia wa Rwanda.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ya vyuo vyetu ni kuzalisha viongozi walio na uchungu na uzalendo na nchi zao wanaokuja kusoma humu nchini na sisi kuzalisha mafisadi wasio na uchungu na uzalendo na nchi yetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh sana aisee ni good comment.

      Delete
    2. UDSM inatakiwa iige vyuo vya Ujerumani,ukifanya mambo ya aibu kama ufisadi,rushwa na mauaji wanakunyang'anya cheti chao.

      Delete
  2. Ni kweli kabisa Anonyomuas wa 10:15

    ReplyDelete
  3. namm umenixahau np UDSM

    ReplyDelete
  4. Ni vizuri sana...

    ReplyDelete
  5. Kumbe na mimi nitakuwa mutu maana niko Udsm

    ReplyDelete

Top Post Ad