Wakati Hata Arobaini Bado Mke wa Marehemu George Tyson Ataka Mali zake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: ShanI Ramadhani na Mayasa Mariwata
Wakati hata siku arobaini hazijatimia, mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo juzi alicharukia mali zake baada ya kuamua kutinga nyumbani kwa marehemu, Mbezi Makonde jijini Dar kwa lengo la kuchukua kila kinachomhusu.

Mdada huyo aliyefunga ndoa na Tyson Agosti 9, 2012 nchini Kenya na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Eugene, alishuhudiwa na gazeti hili Juni 24, mwaka huu saa sita usiku akiwa na ndugu zake na kuanza kugonga geti la nyumba hiyo.

Katika kujua kilichokuwa kikiendelea, mmoja wa mapaparazi wetu aliwasogelea na kuzungumza na Beatrice ambaye alieleza kuwa, lengo lake lilikuwa ni kuchukua mali zake zilizomo mle ndani.
“Ulidhani mimi nataka kuingia kwenye nyumba hii nikae, la hasha! Nimefuata mali zangu tu basi,” alisema Beatrice huku akiendelea kugonga geti hilo.

Wakati Beatrice na nduguze wakionekana kukata tamaa ya kufunguliwa, mara alitokea mwanamke anayedaiwa alikuwa akiishi na marehemu mpaka kifo kilipomkuta na kuuliza aliyegonga geti ni nani, alipotajiwa jina la Beatrice alisema: “Eee, Beatrice, usiku huu umekuja kutafuta nini?”
Beatrice: Nina shida, naomba ufungue tuongee.

Mwanamke: Hatuwezi kuongea usiku huu, uje kesho asubuhi.
Beatrice: Nakuomba ufungue tu, nimekuja kuchukua mali zangu nilizoacha humo ndani na nimekuja na gari kabisa la kubebea.

Mwanamke: Mali gani, humu hamna chako na kama una kitu chako humu, fuata taratibu.
Beatrice: Nimefuata taratibu, nipo na mjumbe hapa.
Mwanamke: Ndiyo nasema mje kesho asubuhi na mapema mtanikuta.
Baada ya mwanamke huyo kugoma kufungua, mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Sabina Mawanda aliwashauri waondoke na kurudi tena asubuhi lakini inadaiwa walipofanya hivyo walikuta nyumba imefungwa na hakukuwa na mtu.
GPL

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kufa kufaana dah

    ReplyDelete
  2. marehemu alidhani ataishi daima ndio matunda yake sasa wanawake wake wanataibika. very selfish kwanini asiandike urithi mapema hao watoto watalelewa vipi khaaa

    ReplyDelete
  3. wanawake 3 kweli kazi mpaka kelo kumbe alikuwa kicheche ivyo penginr mboni naye alikuwa bwana wake maaana

    ReplyDelete
  4. RIP Ila nimemshusha thamani mtu Wa kubadilisha wanawake

    ReplyDelete
  5. Huyo mwanamke nae atakufa soon anajiona mjanja kugoma kumpa mwenzie vituvyake.cheza na Israel atamtembelea soon

    ReplyDelete

Top Post Ad