HITILAFU: Abiria 48 wa PrecisionAir Wanusurika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Ndege ya Shirika la PrecisionAir iliyokuwa imeruka kwa safari zake kutoka Mwanza kwenda Nairobi nchini Kenya kupitia Kilimanjaro jana, imelazimika kutua kwa dharura baada ya kupata hitilafu ikiwa angani.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege hiyo namba 5H-PWC ATR 72, zilieleza kuwa tayari walikuwa wameruka lakini baada ya muda mfupi waliambiwa hawawezi kuendelea na safari kutokana na ndege kupata hitilafu.

Baada ya kuruka, ndege ilitaka kukunja magurudumu kwa ndani ikashindikana hali iliyomlazimisha rubani kuzunguka eneo la uwanja huo, huku akijaribu kuyarudisha bila mafanikio na kuamua kutua kwa dharura.

Alisema abiria 48 waliokuwa kwenye ndege hiyo hadi jana saa 12:00 jioni walikuwa wanasubiri nyingine ili kuendelea na safari.

Akizungumza kwa simu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Ester Madale alisema hitilafu hiyo ilikuwa ya kawaida hivyo haikuwa na madhara.

Madale alisema iliruka saa 7:54 mchana kwenda Kilimanjaro, lakini baada ya kuruka magurudumu yalishindwa kujikunja kurudi ndani hivyo rubani alijaribu kuyarudisha ikashindikana, hivyo akalazimika kutua kwa dharura.

“Hitilafu hiyo ni ya kawaida, wahandisi wetu waliangalia hitilafu hiyo na saa 9:15 alasiri walifanya majaribio kuirusha na imetua, hivyo siyo tatizo kubwa la kawaida,” alisema Madale.

Matukio ya karibuni

Desemba 13, mwaka jana ndege ya PrecisionAir aina ya ATR 42-600 ilipasuka magurudumu  manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA, miongoni mwa abiria waliokuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.

Julai 24, 2012 ndege ya shirika la Precision Air magurudumu yalipasuka wakati ikitua Uwanja wa Ndege mkoani Kigoma.


Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Serikali ya nchi hii ichukue hatua dhidi ya shirika hili la ndege.hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii alitoa taarifa kuwajulisha precision Air juu ya kuisha matairi kabla na baada ya kusafiri na ndege ya shirika hili,majibu aliyopewa na mmoja wa wafanyakazi wa shirika hayakuwa ya kuridhisha kuzingatia usalama wa abiria.Kwa kifupi tairi mbili za nyuma za ndani zilikuwa kipara kabisa kiasi cha nyuzi kuwa nje.

    ReplyDelete

Top Post Ad