Aibu! Wanafunzi wanaswa GESTI Wakijiandaa kula URODA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14  (darasa la saba), wa kiume miaka 15 (kidato cha kwanza) mjini Morogoro wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya Mungu.

Tukio hilo lililojaza umati lilijiri hivi karibuni katika gesti hiyo ambayo inadaiwa haina usajili halali iliyopo jirani na soko.

Habari zinasema kuwa, siku hiyo denti wa kike alitumwa sokoni na mama yake kununua mahitaji mbalimbali ya chakula lakini alichelewa kurudi.

Ikazidi kudaiwa kuwa mama yake alimfuatilia huku akiwauliza watu, ndipo mbeya mmoja akamtonya kuwa amemwona binti yake akiingia gesti hiyo na kivulana! Mama wa watu, akiwa na mshangao, naye alizama ndani na kuwakuta chumba namba 5.

Mwandishi alifanikiwa kutinga eneo la tukio wakati wa sekeseke hilo na kuzungumza na mashuhuda wawili, Asha Chande na Tausi Omary. Alipowahoji walisema waliwaona wawili hao wakizama ndani ya gesti hiyo na walishangaa kwa nini walikubaliwa kwa vile wote ni watoto.

”Baada ya muda mama mmoja mtu mzima alifika hapa akiwa amefura  kwa hasira, akadai binti yake aliyemtuma sokoni ameingia gesti, mara na yeye  akaingia ndani, alimkuta yupo na mvulana huyo huku mfuko aliotumwa nao sokoni binti wa kike ukiwa chini ya kitanda.

“Aliwafurumusha, kivulana kimekimbia zake na huyu binti ndiyo kama hivi. Mbaya zaidi hapa ni sokoni, watu wameacha biashara na kujaa,” alisema Tausi.

Wakati sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walitaka kumwangushia kipondo denti huyo wa kike kwa kitendo chake cha kuacha alichotumwa na kuzamia kwenye mapenzi akiwa bado mwanafunzi.

Baadaye polisi  wa pikipiki walifika na kumchukua denti huyo kwa lengo la kumuokoa na kipigo na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ambapo ilidaiwa kuwa polisi walishauri wazazi wa watoto hao wakayamalize nyumbani.

Juhudi za mwanahabari wetu kutaka kuzungumza na mlinzi wa gesti hiyo ziligonga mwamba baada ya muda mwingi kufunga geti kubwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad