Ali Kiba Amefunguka Kuhusu Mambo Yaliyomkwaza Kutoka kwa Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba amefunguka kuhusu mambo yaliyomkwaza kutoka kwa Diamond miaka michache iliyopita baada ya mkali huyo kutoka na wimbo wa ‘Kamwambie’ uliogeuka kuwa wimbo wa taifa wa Bongo Flava kwa muda. 

Akiongea na kipindi cha Mkasi, Ali Kiba ameeleza kuwa yeye ndiye mtu aliyepitisha ombi la Diamond kurekodi katika studio za SharoBaro kwa kuwa wakati huo alikuwa mdau mkubwa katika uongozi wa studio hizo lakini matokeo yake yalimgeukia hadi kuamua kujitoa katika team hiyo. 

Ameeleza kuwa mara baada ya Diamond kutoka na Kamwambie, aliona gazeti moja lililokuwa lililomkariri akisema kuwa yeye ndiye ‘fimbo’ ya Alikiba na amekuja kumfunika. 

Hata hivyo maneno yaliyowekwa kaitika gazeti hilo yalianza kuaminika kwa Ali Kiba baada ya kukutana nae mara kadhaa kwenye shows. 

“Lakini nilishawahi kukaa na Diamond katika mikutano ya Shows ambazo tunaitwa pamoja wasanii na nini na nini. Mimi napendaga kuongea nae kama mdogo wangu kwa sababu the way nilivyokuwa nikimtreat ni kama wadogo zangu wengine akina Bob Junior akina nani… Nilimsikia akiongea sana kwamba nimekufunika kwenye show fulani, nimekufunika kwenye show fulani. Kwa kweli the way nilivyokuwa nikimtreat kama mdogo wangu. Kwa hiyo yeye alikuwa ameconcentrate sana katika kunifunika.” Alieleza Ali Kiba. 

“Mimi sio mtu wa kumind sawa. Kwa hiyo alivyokuwa anaongea anajifurahisha. Hata kama amenifunika mimi nilikuwa naweza kumpigia makofi vilevile. Si nataka afanikiwe. Kwanza nafurahi. Napenda sana challenge. Inakufanya unaaamke.” Aliongeza. 

Kujirudia kwa neno ‘kufunika’ kila walipokuwa akikaa na Diamond kuligeuka kuwa kero kwa Ali Kiba huku mengine yakipenya kutoka kwa watu wake wa karibu. 

“Kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinahappen tukiwa karibu hivi, ni hivyo vitu ambavyo akizungumziwa nimekufunikaa..nimekufunika. Nikawa nikitoa video nasikia maneno, kwamba ‘Ali amesikia maneno nimetoa hii na yeye ametoa hii’. Mi sijawahi kumsikia mwenyewe akisema. Ila watu wake wa karibu wa karibu wanakuja wanasema. Unaweza kumjua mtu tabia yake kwa kumuangalia, kwa kuishi nae.” 

Ali ameeleza kuwa hata baada ya kuamua kukaa kimya amlee mwanae wa kiume alisikia tena maneno kutoka kwa mwimbaji kwa Diamond kuwa amemkimbia. 

Hata hivyo, hii ilikuwa story ya zamani ambayo wengi wanaweza kuwa nayo lakini ikamhusu mtu ambaye kwa sasa amekuwa rafiki wa kudumu. 

Hivi karibuni Ali Kiba alisema kuwa hana tatizo lolote na Diamond na kuwataka watu wasimgombanishe na msanii huyo. Ni muda wa biashara. Yaliyopita si ndwele (maradhi) tugange yajayo kwa maendeleo ya Bongo Flava. Kilichobaki ni ushindani wa kibiashara kama alivyosema Babu Tale
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waache acha umbea mwandishi hunajipyaaa

    ReplyDelete
  2. kiba punguza kumzumguzia domo fanya kazi kwa bidii.unapotumia muda mwingi kuzungumza ya domo inaonyesha kweli kakufunika,mbona yeye hazunguzi juu yako?hao wanaokuletea habari unawaamini vipi?usipoteze muda mwingi kwa domo fanya kazi kijana.acha kukimbiliakimbilia media,tunga nyimbo dogo mbona uwezo unao....

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWELI MDAU HAPO JUU,HUYU KIBA ANATAKIWA KUFANYA KAZI NA SI KUTANGATANGA KWENYE MEDIA,AANZE KUKATAA MASWALI KUMHUSU DIAMOND SABABU ANAONYESHA INFERIORITY COMPLEX KWA DOMO,UKIONA DOMO HATA KWENYE UKURASA WAKE WA INSTA UTAONA MARA NYINGI ANAONYESHA KAZI ANAZOFANYA LAKINI KIBA
      UTAONA ANAPOSTI INTERVIEW KWENYE MEDIA,YAANI NADHANI NDO ANAONGOZA KUFANYA INTERVIEW NA HAIJAWAHI TOKEA ANASTAHILI TUZO KWA HILO. KA UTADHANI UNDERGRAUND?? AMEKAZANIA DIAMOND NILIMSAIDIA SIJUI AREKODI MANENO KIBAO.ACHA HIZO KIBA FANYA KAZI NA MEDIA ZITAKUTAFUTA TU POPOTE ULIPO ILA KWA SASA KWA MWENDO HUO WEWE SI LEVEL YA DOMO HATA SIKU MOJA.

      Delete
    2. Kiba upo juu Sana. Achana na domo.

      Delete
  3. Ana jipya aliy kiba

    ReplyDelete
  4. Ushauri wa bure kwa ali kiba mi nadhani ungeacha rasmi kumzungumzia domo, kama unaulizwa swali kuhusu huyo domo katakaa kulijibu na concentrate kutoa mziki, maana juzi umesema hutaki watu wakukosanishe na domo sasa unamuongelea wa nini?

    ReplyDelete
  5. acheni kucoment usenge ally k bila kuulizwa angemzungumzia wote mnadinywa na domo nyie hapo juu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata kama anaulizwa, anatakiwa amtahadharisha anayemuhoji kuwa hapa sitaki maswali yanayo muhusu Dangote full stop. Kwani hajisikii vibaya kumzungumzia mtu ambaye hana mpango nae, Dangote amehojiwa mara nyingi tu lakini sijasikia akimzungumzia Kiba, hata wakimtega yeye anapotezea.

      Delete
  6. KIBA KULA KIMYA MKALI...
    ACHANA NAE MCHUMBA TU HUYO.

    ReplyDelete
  7. ANAWEWESEKA aendelee kulea watoto wenzie wanachanja mbuga kwani akiwaambia wanahabari msinihoji kuhusu Dai watalamzimisha? Watu tunamfahamu kila sikuinterview utafikiri underground anataka kujulikana?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anaitwa kwa ajili ya interview,hajipeleki.kachambe ulale

      Delete
    2. Hiyo interview anayoitiwa ni kwa ajili ya DOMO au?

      Delete
  8. Kiba anajibu anapoulizwa na media,haongei kama anavyoongea Domo.

    ReplyDelete
  9. ww ali kiba fanya kazi ndo iongee c ww kila cku kumzungumzia nasib..mwenzio anachanja mbuga ivo..

    ReplyDelete

Top Post Ad