IRENE UWOYA Kumpeleka NDIKUMANA Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BINTI aliyejaliwa uzuri wa sura anayeng’ara kwenye filamu za Kibongo, anamshawishi mumewe Hamad Ndikumana aje kucheza Yanga ya chini ya kocha, Marcio Maximo.

Ndikumana ambaye kwa sasa anaichezea Vital’o ya Bujumbura, Burundi ameweka wazi kwamba binti huyo, Irene Uwoya ambaye ni mkewe ni shabiki wa Jangwani na amekua akimshawishi kila mara kwamba atue Jangwani ili awe naye karibu zaidi kwani hana mpango wa kuondoka Dar es Salaam kwenye kazi zake za filamu.

Mchezaji huyo amekiri kushawishiwa mara nyingi lakini alisema hawezi kujipeleka Yanga mpaka timu hiyo itakapomfuata, kama hiyo haitoshi aliongeza kwamba anaogopa kuishi Dar es Salaam kutokana na mambo ya ushirikina yaliyomtokea alipoanza maisha na mkewe ambaye ameshangaa watu wanaozusha kwamba wameachana.

Ananitaka nije kucheza Tanzania alikuwa ananiambia nije Yanga, unajua anaipenda sana Yanga lakini nikamwambia mimi ni mchezaji ninayejiamini siwezi kuja kuomba Yanga wanisajili acha waje wao tuzungumze, yuko tayari kufanya hata ushawishi kwa wadau,” anasisitiza Ndikumana ambaye awali alikuwa akiichezea APOP Kinyras Peyias ya Cyprus.

Ndikumana alisema kilichomtoa Cyprus na kuja Burundi pamoja na uhusiano wake na Uwoya.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tutamjaribu kwanza, kama anafaa tutamsajili, kama hafai tutawaachia simba maana wananjaa sana na wachezaji wa Yanga!

    ReplyDelete
  2. mtt kapendeza kweli nakitaulo lakini! dah!

    ReplyDelete
  3. Ugonjwa mtupu,kaonga ili aandikiwe stori vizuri,ndikumana aliuguaga saaana wakadai ni uchawi,ndo uwoya akaona gozigozi kuuguza mgonjwa akamkimbiaaaaaa

    ReplyDelete
  4. kwanin usiende kukaa nae uko burundi..mana iyo klabu ya vital"o ni nzuri kuliko ht iyo yanga yako

    ReplyDelete
  5. Uyu mtoto irene atakua simba huyu... mume alikuoa akiwa bonge la beki.. katauti!! Leo umemtia stress kibao kweny misukosuko ya ndoa mpaka kipaji cha mpira kikafa, akatimuliwa cypruss sasa hv vitaloo ndo wanamstiri ndugu yao.. leo hii utuletee yanga???? Wacha masihara umetumwa wewe na simba.. anapigwa matobo kichizi huko kagame cup.. leo hii asimame na yule mviziaji boya asiejua mpira tambwe itakuaje?? Ungemleta kipindi kile!!

    ReplyDelete

Top Post Ad