Gari lililobeba Maiti Kumi za Mafunzo Laua Wawili Mikese

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10  za watu kwenda katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara, wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.

Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.

Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.

Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi wa Ifakara, wilayani Kilombero.

 Mbao  aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.

Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya mabaki ya miili ya binadamu kugunduliwa ikiwa imetupwa katika dampo moja lililoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi hii miili inayofanyiwa mafunzo haina ndugu ama mpaka inazagaa kila kona

    ReplyDelete
  2. Hizo maiti za mafunzo hazikuridhia kwenda ifakara ndo mana zikaamua zisababishe ajari, amini nakuambia hata Rais ukimwambia Ikulu ihamie dodoma atakataa Dar kuzuri jamani

    ReplyDelete

Top Post Ad