Manji: Tutapigania haki ya kusaka chetu kwa Okwi mpaka kieleweke

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siku moja baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi, hii leo uongozi wa Dar es salaam Young Africans ukiongozwa na mwenyekiti Yusuph Manji umeibuka na kukana kumpa barua mshambuliaji huyo ya kuvunja naye Mkataba na imesema mshambuliaji huyo Mganda, amewahadaa Simba SC.

Mwenyekiti huyo wa Dar es salaam Young Africans amesema tayari wameshaliandikia shirikisho la soka nchini TFF na kuomba ifanye mambo mawili, moja ni kumfungia Okwi kucheza soka na la pili ni kuifungia klabu ya Simba.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Dar es salaam Young Africans, Yusuph Manji amesema wametoa siku saba kwa TFF kufanya hivyo.

Manji amesema, iwapo TFF itashindwa kutekeleza hayo ndani ya siku hizo saba, wao watahamia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambako kama hawatafanikiwa pia, watahamia Mahama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).

Manji amesema leo asubuhi wametuma malalamiko yao kimaandishi TFF na pia wanamdai Okwi fidia ya dola za Kimarekani 500,000 (Sh. Milioni 900) kutokana na kuvunja mkataba na wao.

“Tunataka Okwi afungiwe kucheza soka na Simba ifungiwe kutokana na kumsainisha Okwi. Tumeipa TFF siku saba ifanyie kazi malalamiko yetu,” amesema Manji.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba, kabla ya jana katika malalamiko ya awali waliyotuma TFF, walitaka Okwi awalipe dola 200,000 (zaidi ya Sh. Milioni 340,000), lakini baada ya Simba kutangaza imemsajili jana, dau limepanda.

Manji amesema kwamba Yanga haina ubaya na Simba, bali watani wao hao wa jadi, wamefanya vibaya kumsainisha mchezaji huyo bila kuwasiliana nao.

“Simba SC walipaswa kuja kutuuliza kabla ya kumchukua Okwi, na wala sisi hatuna ugomvi na Simba, endapo watafungiwa au kushushwa daraja wasilie na Yussuf,”amesema.

Amesema Yanga haitatetereka kwa kuondoka kwa Okwi, shida ni kwamba taratibu hazikufuatwa. “Yanga imeachana na walimu na wachezaji mbalimbali kama Freddy Mbuna, Nsajigwa Shadrack kwa amani. Na nilisema mapema katika mkutano wa Juni, kwamba Okwi kama hatarudi, tutasajili wachezaji wengine wazuri, nimesajili Coutinho (Andrey) na Jaja (Geilson Santana),”amesema Manji.

Jana Okwi ametangaza kurejea Simba SC kwa mkataba huru wa muda, akida Yanga SC imempa barua ya kusitisha mkataba naye pamoja na kumshitaki TFF.

Okwi alisema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.

“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”alisema Poppe.

Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 (Sh. Milioni 500) Etoile du Sahel ya Tunisia.

Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.

Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.

Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.

Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.

Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.

Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho jana baina ya mchezaji huyo na Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.

Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Manji usimwachie huyo mburula, ameshakula fedha nyingi sana, lazima akione chamoto ili iwe fundisho kwa wengine, kwani yeye ninani, na TFF tunakuombeni mumu adhibu huyu jamaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisaaaaaaa! TFF wasibabaishe ukweli juu ya huyu Okwi,
      ni msumbufu hata ukiangalia mahudhurio yake,yeye akishapata hela anakuwa
      na jeuri sana,wachezaji wa kigeni wote wanocheza Tz wana heshimu sheria za timu zao lakini sio Okwi,Mpumbavu huyu.

      Delete

Top Post Ad