Mashosti Wawili wa Wema Sepetu Wanaomsaidia Kula Ujana Watifuana Kwa Matusi, Nusura Wazichape Nyumbani Kwa Wema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nice Chande, Wema na Aunt
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na shostito wake Nice Chande, juzikati walijikuta walitifuana kwa matusi makali ya nguoni nyumbani kwa rafiki yao Wema Sepetu ‘Madam’ anayeishi mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Chanzo makini cha habari kilichokuwa nyumbani kwa Wema, kililidokeza gazeti hili kuwa waigizaji hao wakiwa na rafiki yao mwingine, walianza kutukanana kwa jambo ambalo halikuweza kubainika mara moja, huku Madam akijitahidi kuwasuluhisha bila mafanikio.

Wakiwa na dalili zote za kubugia kiburudisho cha kutosha kilichowafanya wasione vibaya kupaza sauti za matusi mbele za watu, marafiki hao walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuendelea kutukanana kana kwamba hawana akili nzuri.

Baada ya kuona watu wameanza kukusanyika usiku huo ili kushuhudia sinema hiyo, Aunt, Nice na rafiki yao walijipakiza kwenye gari, huku Aunt akiwa nyuma ya usukani na kuanza safari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake, Mwananyamala, lakini safari yao iliishia hatua chache mbele baada ya dereva huyo kulitumbukiza mtaroni gari hilo.

Kuona hivyo, watatu hao walishuka na kuanza kurudi tena nyumbani kwa Wema, ambaye aliendelea kuwasihi lakini wakiendelea kushambulia kwa maneno makali, kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa ndiye chanzo cha ajali ile.
Nyumbani kwa Wema, wasanii hao walimuomba msaidizi wake, Petit Man aende kuwasaidia kulinasua gari hilo mtaroni, kazi ambayo ilifanywa na vijana wa mtaani hapo waliolipwa kiasi cha shilingi 50,000.
Hata hivyo, baada ya gari hili kuletwa kwa Wema, si Aunt wala Nice waliokuwa tayari kulipanda, hali iliyomlazimisha mwenyeji wao kupiga simu kuita teksi, ambayo pia baada ya kufika, Nice alikataa kuipanda, badala yake Aunt na shostito wao mwingine ndiyo waliingia ndani na kutokomea.

Baada ya kukubaliana kuwa gari lile lilale hapo, Wema alimtaka Nice kuingia ndani, lakini aligoma, akidai anataka kuongea na baby wake kwa njia ya simu, lakini mwenyeji wake aliamua kuita teksi nyingine ambayo ilifika na kumchukua.
GPL

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tayarisheni mashamba mkalime mvua zi karibu.

    ReplyDelete
  2. Domo! Domo!
    Kumbuka kuwa wewe ni kutoka familia masikini sana.
    Ishi maisha yako na fanya maamuzi ukifikiri miaka ijayo kwani kipato cha muziki hasa wa kibongo akitabiliki
    Na mama ubaya ni mtu wa showoff na matumizi makubwa nawe huna chanzo cha uhakika cha mapato
    Huyo mama ubaya sio wife material hata Yusuph Bakhresa hawezi thubutu pamoja na uhakika wa kipato kwake
    Ndoa sio swala la mzaha eti ulidhishe so called team wema
    Kweli masikini akumbuki alikotoka hivyo bila juu zako binafsi huyo mama ubaya hangekung'ang'ania
    Kumbuka yeye ujiweka kwa watu wakipata mafanikio kama ilivyo kuwa kwa tid kanumba blue chaz baba etc.
    Jifunze ulaya wanawake wa showoff ni mabingwa wa kudai talaka ili wagawane mali na superstar alikichuja kama ilivyotokea kwa Tyson, Michael Jordan to mention few

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mdau,wazuri kwa Domo ni wale aliokuwa nao tangu enzi za ule wimbo wake ''Kwetu mbagala''

      Delete
    2. Nani akawe msukule,

      Delete
    3. mmmmmmh cjui dada cjui kaka unaongea balaaa adi mengine tulikuwa hatuyajui kama hawajaelewa tu ndio baaasi tena

      Delete
    4. Mdau Wa 11:44 unaniboaa Hilo limeseji la kukopi na kupaste unalituma kila blogu we unaonekana una chuki binafsi na Wema.

      Delete
    5. Atakuwa ni andunje Penny au Halima kimwana mapengo

      Delete
  3. Huyo mmoja hapo juu anafanya kazi Bank lakini kujitoa Akili

    ReplyDelete
  4. domo anawagonga wote hawa, walikuwa wakimgombania

    ReplyDelete
  5. Out of topicccccc,wadada Wa mujini keen chonjoooo,kwenye blogu ya Sintah kuna mtu katumbua JIPU, kwenye comment,eti kasema Lulu Michael anachepuka na dogodogo Wa Shamim Mwasha,huyu lulu ana akikisha anatembea na mwanaume yoyote mwenye hela.,anamwanaume Wa mererani lakini badoooo aridhiki.

    ReplyDelete
  6. Kila mtu analysis Abdul Nsembo,wanamvizia kweli magomeni,nikiwataja hapa shamim atakuwa na maadui kibao ngoja niuchune,wanaume wenye hela wanakindwa kweliii na wabongo movie

    ReplyDelete
  7. ila udaku mwingine ni kama upuuzi tu kutuletea uku sas uwo ungovi unatuhusu nini bona auandiki vitu vya maana nyie kwan kuna watu ambao awangomban unataka kumaanisha wew ujawai pishana na mtu kiswaili ebu muagalia.udaku wa kupost ban lasivyo mim na weza kuwakimbia

    ReplyDelete

Top Post Ad