Zitto Kabwe Kwa Mara ya Kwanza Aongelea Uhusiano Wake na Diva Loveness, Amkana Diva

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KWA mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.

Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.

Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.

Alisema anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.

“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.

Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.
GPL
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aibu take diva kutwa kuchwa nimetembea na mbunge na prezoo....kwa mwanaume anayejielewa haez kukubal kuwa anatoka na yule punguani....inaonekana wanavyomtokea wanadhan no MTU na akili zake wakikaa nae kidogo ndo wanagundua kuwa ni SAA mbovu gegedu

    ReplyDelete
  2. Daah,sijui ndio tusemeje au imekaaje mwanamke anapojisifia kutoka na fulani, halafu fulani mwenyewe akukane.kwamba huna hadhi ya kuwa nae kiasi anaona aibu kukubali kuwa anatoka na wewe?au?Kwani, kwa nini kila ukipata mwanaume lazima utangaze ili Watu wote wajue,ni kuto-jikubali,kuto-jitambua ,AU?

    ReplyDelete

Top Post Ad