AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mtoto mwenye umri wa miaka sita amefariki baada ya kukanyagwa na gari la mamake.
Bolutito Shodipe mwenye umri wa miaka sita aligongwa na mamake aliyekuwa anajaribu kuegesha gari lake nje ya kituo cha treni cha Hounslow West Tube nyakati za asubuhi Jumatano wiki hii.
Juhudi za kuokoa maisha ya Bolitito katika eneo hilo ziliambulia patupu kwani alisemekana kuaga dunia alipofikishwa hospitalini.
Taarifa kutoka kwa familia ya Bolitito ilisema kuwa wanajaribu kuikubali hali iiliyowakuta kutokana na ajali hiyo mbaya.
Familia hiyo inayoishi eneo la Hayes Magharibi mwa London, iliongeza kusema: "Bolutito alikuwa mtoto wetu wa kwanza na alikuwa nuru kwetu. ''
"alikuwa mrembo, mwenye maadili mema, na mpenzi wa Ballet, na tutamkosa sana.''
Polisi walithibitisha kwamba kifo cha mtoto huyo kilikuwa ajali kwani walifika wote katika kituo cha treni na mamake, ila mtoto aligongwa na kufariki wakati mama akijaribu kuegesha gari lake.
Polisi wanachunguza tukio hilo.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Jamani dunia hii pole sana mama, mungu atakupa mwingine.
ReplyDeleteDaah! walikuwa jirani zangu,nilimuacha akiwa na miaka 2.
ReplyDeletewatu wazuri sana ,R.i.p B
Rest in Peace Cute baby! Pole sana kwa mama na Mungu akutie nguvu. Amen
ReplyDelete