UKAWA Wajitoa Rasmi Kwenye Mchakato wa Katiba, Wanazuoni Wawapa Somo.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KAMA ndivyo, huenda Bunge Maalumu la Katiba, linalotarajiwa kuanza awamu ya pili ya vikao vyake keshokutwa mjini Dodoma, litafanyika bila ya kuwa na wajumbe kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Hali hiyo inatokana na kauli ya Ukawa, inayoundwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani na wafuasi wao, kwamba hawatashiriki katika Bunge hilo na kwenda mbali zaidi, wakidai hawana mpango wa kuwa na vikao vya maridhiano dhidi ya wenzao wa chama tawala, CCM baada ya kikao kingine cha juzi, kilichokuwa cha nne, kukwama.

Kauli ya Ukawa ilitolewa jana, mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda umoja huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Kwa pamoja, walisema wameridhia kujiweka kando katika Bunge na vikao vya maridhiano. Chama cha NLD kinachoongozwa na Dk Emmanuel Makaidi, nacho kimejiweka kando.

Mbowe alifafanua kuwa baada ya kikao cha nne cha maridhiano kati ya umoja huo na CCM, kilichofanyika juzi chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuvunjika, wametafakari kwa kina na kubaini kurejea bungeni kuendeleza mivutano, hakutakuwa na tija kwa Taifa.

“Hivyo tumeazimia kutorejea tena katika Bunge la Katiba wala kushiriki mazungumzo yoyote kuhusu suala hilo, kutokana na ukweli kuwa mazungumzo haya yaliyovunjika, yalikuwa ya kuwezesha kupata Katiba bora, lakini CCM waliyafanya kuwa yenye maslahi ya chama chao, siyo Taifa.

”Na baada ya awamu nne za vikao vya mazungumzo kati yetu na CCM, Ukawa tunatangaza kwamba hatuko tayari kuendelea na mazungumzo na CCM wala kurudi katika mkutano wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa kuwa kufanya hivyo ni kusaliti maoni ya wananchi na kutumia vibaya fedha za umma,” alisema Mbowe.

Kauli ya CCM Hata hivyo, kwa mara nyingine jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema chama chake hakijashangazwa na uamuzi huo, kwa kuwa walifahamu Ukawa hawana hoja za msingi, hivyo wamekimbia aibu.

“Hata kwenye vikao, hawakuwa na kitu kipya, ni malalamiko tu huku wakishindwa kujenga hoja, kwa hiyo tulijua hawa wenzetu lazima mwisho wa siku wakimbie aibu yao…ni aibu tu imewashika, ndiyo maana wamepatafuta pa kutokea,” alisema Nnauye.

Wakati huo huo, Mkuu wa Shule ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba amewasihi wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa itakuwa si busara kutorejea bungeni Agosti 5, mwaka huu, badala yake watumie nafasi hiyo kurudi bungeni na kushindanisha hoja zao.

Alisema hayo katika mdahalo wa kutoa maoni na msimamo wa wananchi, juu ya mivutano ya makundi katika mchakato wa Katiba. Mada mdahalo huo ilikuwa ni “Nini suluhisho na wajibu wa makundi katika mchakato wa Katiba”.

Mdahalo huo ulitayarishwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS). Ulifanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, jana.

“Katiba ni ya Watanzania, siyo wanasiasa wa Tanzania, wale waliomo ndani ya Bunge la Katiba ni wajumbe tu ambao wametumwa, kwa maana hiyo hata kama ni wanasiasa wako kule ni lazima wasahau vyama vyao na kuupa kipaumbele Utanzania wao,” alisihi Profesa Lumumba.

Alisisitiza kuwa Tanzania ina nafasi ya kipekee na kihistoria barani Afrika ya kupata Katiba mpya, bila mapigano ya aina yoyote. Alisema litakuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha, ikiwa amani iliyopo hivi sasa, itatumiwa na wanasiasa wenye ufinyu kwa mitazamo yao ya siasa na kusababisha mapigano.

Profesa Lumumba alisema Rais Jakaya Kikwete aliona umuhimu wa Tanzania, kuwa na Katiba mpya na aliamua kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba hiyo.

Profesa huyo alisema Rais Kikwete anastahili kupongezwa na kila mtu, kwa hatua yake hiyo kubwa na nzuri kwa Taifa la Tanzania.

Alisema Tanzania inatakiwa kujifunza kuhusu uandikaji wa Katiba mpya, kutokana na makosa yaliyofanywa na nchi nyingine, ambako yalitokea mapigano
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UKAWA ni wasenge, na wala wasirudi tena bungeni, wakauze gongo wanazozinywa. Sie wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho. Tunasubiri bungeni wamalize yao na sie ndio tuamue tuseme ndio (kama katiba imefata maoni yetu) au hapana (kama haijafata maoni yetu).

    ReplyDelete
  2. Wewe anonymous 9.10 ndio msenge.sikutaka nitumie lugha hiyo ila nimelazimika kurudisha ulichosema.kiufupi wewe ni mjinga wa mwisho kabisa.wewe ndio unahongagwa ubwabwa wa siku moja unampigia kura mgombea uongozi mbovu halafu baadae unateseka kwa miaka kumi kwa mlo 1.cha kushangaza huishi kulalamika kila siku huku mitandaoni kwamba maisha ni magumu.......Unajua hiyo katiba inayopigiwa chapuo na wezi wa ccm itatumika kukusulubu wewe na vizazi vyako kwa miaka mingapi ijayo??au unabwabwaja tu humu mitandaoni kwa hicho kisimu chako cha mchina ulichopewa zawadi.unajua kwamba hao UKAWA unaowatukana wanapigania haki za kina nani au unaropoka tu kama upo chooni?!kesho na keshokutwa wanao na wajukuu zako watakuja kufukua maiti ya na kuipiga mawe kwa wewe kutetea na kuongea upuuzi kama huu unaofanywa na majambazi wa ccm kwa watanzania milioni 50. Wale wezi wanaingia pale bungeni kutumbua pesa zetu za kodi bila sababu yoyote wakati watanzania wanakufa kwa umasikini kwa kukosa dawa hospital,maji safi na salama,elimu bora,miundombinu imara,zana za kilimo bora na mambo mengine halafu wewe mpuuzi unaongea ujinga wako hapa.PUMBAVUUU KABISA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani mdau hapojuu umeongea point sana.jamani watanzania wengine sijui wamelogwa au nikukosa akili ukawa Wako right.misinachama ILA ccm nimewachoka namafisadi wake wote,lbda watoke madarakani hao wapuuzi wajewengine tuone mabadiliko.lkn ccm si chama tena kile cha nyerere kimekuwa chama cha mafisadi tu.ingekuwa tunakubali haki basi mungu angetuongoza nchi isingefikiahapa tulipo.mfano kushinda ashinde mwingine Kura anapewa mwingine.uwizi,ubinafsi ahh.muogopeni mungu nyie mafisadi

      Delete
  3. katiba haibadilishi hali ya maisha usidanganywe na wana siasa ndugu yangu

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu hapo juu 10:27 umeongea point sana watanzania sisi ni wagumu kuelewa na ndio maana viongozi wanatumia hiyo chance kutuburuza!sasa kama huyo jamaa anavyoropoka unajua kabisa uwelewa ni mdogo halafu wengi wetu tunaangalia leo na kesho tuu na sio miaka 10 au 20 ijayo ndio upumbavu wetu sisi!

    ReplyDelete
  5. wewe ndio umedanganywa na wanasiasa uchwala tena wa ccm aliyekwambia katiba haibadilishi hali ya maisha nani?!sasa kazi ya katiba nini?!basi wasingekaa vikao kujadili kama ndio hivyo!tatizo lako wewe unawasikiliza viongozi wa ccm ambao wengi ni mambulula na wako kwa ajiri ya maslahi yao binafsi!

    ReplyDelete
  6. Lumumba aliisoma Rasimu ya pili na kusikiliza hotuba ya JK wakati wa ufunguzi wa Bunge la Katiba?

    ReplyDelete
  7. Naomba ufafanuzi kwani kuna suali linanitatiza Kwani wale wanaosema serikali mbili wamekiuka sheria yoyote ya mchakato wa katiba mm nahic maoni ya wananchi wanautaka muungano tume ndo ilochambua kuhusu serikali ngapi lkn wananchi wametoa maoni tafauti kwani katika suala la muungano serikali tatu cio akizo la wananchi ni makisio na uchambuzi wa tume. sasa hili suala la idadi ya serikali ni maboresho wa rasimu au ndo uvunjwaji wa sheria ya mabadiliko wa katiba . Nauliza hv kwa sababu akili yngu inavyoniambia suala la idadi ya serikali linaweza kujadilika kwa sababu ni fikira za tume ya mabadiliko ya katiba lkn kuwa na muungano ndo suala ambalo halibadilishiki na ndio maoni ya wananchi
    Naomba ufafanuzi kwa wenye uelewa mkubwa zaidi yngu. Tuache usiasa

    ReplyDelete
  8. Watu hawajui.. hizi serikali mbili tu mtaani huku tunalia njaa mungu anajua.. sasa ije na serikari ya tatu, iwe na mawaziri wake na wala rushwa wake wananchi wa kawaida tutabaki na nn??? Mnaijua gharama ya kuendesha serikali wenzenu hao ukawa wapo ki mahesabu ya uroho wa madaraka zaid kama hamjui cc wananchi wa kawaida tunafata mkumbo bila kufanya tathmini.. ndani ya serikari tatu mahesabu ya kitoto ya chadema wanaweza shika dola tanganyika wkt cuf zanzibar coz kule chadema hawakubaliki.. washua wameshtukia ngoma inabaki serikali mbili.. mm na ww mwananchi mwenzangu wa kawaida tunafata mkumbo kutaka gharama za kuendesha serikali tatu.. mm nataka serikali moja.. baaaaaas!!!!

    ReplyDelete
  9. Hao ukawa wanajitoa mara ngapi? Kwani si'walishatoka siku nyingi.......... hawana jipya, wameishiwa..."WAKISUSA WENZAO TWALA"

    ReplyDelete
  10. Me nawashangaa sana hawa ukawa mnabembelezwa hivyo kwani nyie nani kwani mnataka nn haya mbona hamsomeki jmn wananchi tuwaeleweje hamtaki kurudi bungeni halafu mnakuja ktaani mnasambaza sumu mnataka nn lkn hembu jaribuni kuheshim wananchi wenu waliowachagua na mpo hapo mpk sasa lkn hatuoni mnachogomea kurudi??? MUNGU TUNAKUOMBA UTUFUNULIE KIONGOZI MWENYE NIA NZURI NA HII NCHI MAANA WALE TUNATAKA KUWAAMINI HATUWASOMI KABISAA!

    ReplyDelete

Top Post Ad