Bilionea Ampangishia Lulu Michael Jumba la Kifahari, Ampa Jeuri ya Pesa Kuwazidi Wema na Kajala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Hamida Hassan, Gladness Mallya na Musa Mateja.
Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari.

TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.

Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.

Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu.
“Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi,” alidai mtoa habari wetu na kuongeza:

“Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu.
“Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav4 New Model analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana na hadhi yake.

ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA, WEMA
“Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala (Masanja) na Wema (Sepetu) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo.”

LULU LAIVU!
Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV, Lulu alionekana ndani ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani.Mjengo huo una makabati makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia kwenye duka la nguo (boutique) na viatu kibao.

Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye makabati.“Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri,” alisema Lulu.

BILIONEA GANI?
Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa madini jijini Arusha.

“Kama mtakumbuka, huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna (Maulid) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna.“Hivi unajua kabla ya ishu hiyo, Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama paka na panya kisa tu ni huyo bilionea,” kilidai chanzo hicho.

LULU ASAKWA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na alipopatikana alifunguka:

“Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo yeyote, hayo ni maneno ya watu tu. Unajua watu wanaongea sana, wanadhani mimi siwezi kujimudu,” alisema Lulu kwa kujiamini.
GPL

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. who cares ata angekuwa na gorofa....udaku ni waongo jamani

    ReplyDelete
  2. bogo bwana wenye pesaamekaa kimya wasio nazo kutwa kuhangaika kuonyesha watu wanapesa ,...hizo nguo ambazo anazo lulu anavalishwa tu hakuna la maana hapo wehu nyie...kupokonyana mabwana ndo habari zao za mjini so perthetic...

    ReplyDelete
  3. hivi Husna anaeongelewa ni yule miss au???

    ReplyDelete
  4. muandishi wa hii makala cjui unakaa wapi sijaona mi kama ni JUMBA LA KIFAHARI lol ni nyumba ya kawaida inayopaswa kila mtanzania aishi kulingana na rasilimali tulizonazo Tanzania kungekuwa hakuna ufisadi nyumba kama iyo ya lulu ni maisha ya mtanzania mwenye degree tuu! wajameni ila wee muandishi bonge la mshamba ati bonge la jumba mfyuuu

    ReplyDelete
  5. we mwandishi ulivokua muongo jamani mpaka naskia kinyaaaaa.....una uhakika gani hizo hela lulu kahongwa muwe mnachunguza before anything happen hizo hela alionyesha ciku moja akiwa analekodi kipind cha tmt huyo bwana mmempa acheni kupotosha jamiiii..

    ReplyDelete
  6. Hv bwana huwa anaporwa au yeye mwenyewe akichoka anakula kona, maana kumshutumu lulu tuu kuwa kampora bwana huyo malaya mwenzie, hv husna nae mwanamke haswa wakupendwa au wakuchezewa? Juzi juzi tu huyo husna katimuliwa maeneo ya mikocheni baada ya kwenda kuvamia nyumbani kwa bwana mmoja kamkuta kijana na demu wake kakafukuzwa kama mbwa halafu nilichogundua hv videmu vya mjini havijui kama wanaume wanawachezea tuu kupitia njaa zao za vijisenti na akili zao fupi kutwa kuonyeshana na wakati hawana hata pesa ya kula kutwa kuomba hadi vocha ya buku kwa wanaume, kama huyo anayejiita miss sinza ananjaa mpaka matakoni hata hela ya mandazi inamshinda

    ReplyDelete
  7. Si alikuwa anajenga? Kwa nini asimalizie akakae kwenye mjengo wake wa kifahari kama walivyotangazaga!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmh, kujenga mchezo?mjini shule.

      Delete
    2. hizo hela mbona zilishapostiwa long kwenye mtandao,udaku wenu uzushi tu mmepaste picha.
      alaf hella zamesambazwa juu tu chini mikanga.

      Delete
  8. Bongo mavi wakipimwa ngoma wachache sana watakuwa negative.wote wagonjwa tu.

    ReplyDelete
  9. Ila jamani haka katoto si kaende shule jamani

    ReplyDelete

Top Post Ad