Kwa Utajiri Alionao Kajala Sasa Anaweza Kumwajiri Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka, ungana na Ijumaa Wikienda. Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.

TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’. Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna. “Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar. “Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.

KAJALA AMEHONGWA? Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote. “Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala. Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo. WEMA HALI IPOJE? Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.

Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier. Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka. WEMA ATAFUTWA Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa. SHOSTI WAKE Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo. “Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.

KUMBUKUMBU YA JUZIKATI Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake. Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake. DIAMOND ALINENA Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi. “Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyinyi udaku ni wanafiki sana kwa nn kila ck wema halafu huyo kajala kwa nn asimlipie mumewe fain atoke jela na wema ajifunze matumiz mazur ya pesa

    ReplyDelete
  2. wema ana kazi kweli. akiwa low profile kafilisika.. akijitokeza media hana akili.. mweh pole wema kazi unayo

    ReplyDelete
  3. Nampenda kajala mimi jamani........yuko poa sana,
    mtukane yeye sawa,mumsifie yeye sawa,ni mtu wa ewalaaaaaaaaaaa......... ...... H

    ReplyDelete
  4. yani wema ana kazi akikaa kimya kafilisika...akijionesha anapenda atention mmmmh udaku mna kazi..mwacheni kajala hana lolote anataka nawe awe na jina km la wema sema tatizo nyota kama ana pesa amtoe mumewe jela sasa..sioni hata kipyaaaa hapo

    ReplyDelete
  5. amtoe mmewe alafu aje kumzibia kwa ck.wewe mdau vip wewe acha ushamba kuna binadamu anataka shida.ni huyo mjinga wenu wema!?!?

    ReplyDelete
  6. mmmm hayo ni mambo ya clement na c mwingine c amemuibia wema.bwana.wake actake kujifanya izo hela ni za jasho lake wahelevu tunajua ngoja wabwagane na uyo clement uje uckie kama izo hela atakuwa nazo

    ReplyDelete
  7. kajala atausbiri sana kumuajili wema.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni kweli mkundu wa wema bei kubwa sema anabanwa tu kwasasa

      Delete
  8. Kuna tofauti kubwa sana kati ya dunia ya kwanza na dunia ya tatu....

    ReplyDelete
  9. Ningemwona wa maana angejenga badala ya kujinadi unaishi kwenye mjengo unaolipia $2000.

    ReplyDelete

Top Post Ad