Balotelli Anusurika Kutiwa Hatiani Baada ya Kumtukana Mwanamke Aliyekuwa Akipiga Picha ya Gari Lake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la polisi nchini Uingereza halitomchukulia hatua za kisheria mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool Super Mario Barwuah Balotelli kufuatia madai ya kumtolea maneno makali mwanamke mmoja aliyekua akichukua picha za gari lake.

Balotelli anadaiwa kufanya hivyo kutokana na kuchukizwa na kitendo cha mwanamke huyo ambae alionekana akichukua picha za gari lake aina ya Ferrari juma lililopita.

Taarifa za jeshi la polisi mjini Manchester zimeeleza kwamba hakuna uhalifu wowote uliotokea na kumuhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambao umewasilishwa kwao ama kurekodiwa.

Hata hivyo imeelezwa kwamba mwanamke anaedaiwa kutolewa maneno makali na Baliotelli hakuwasilisha malalamiko katika jeshi la polisi na ndio maana ripoti ya jeshi hilo imeonyesha hakuna lolote linaweza kumfika Balotelli.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad