Mwandosya: Kumkejeli Warioba ilikuwa mbinu ya kupata ushindi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya amesema kutumia lugha ya kejeli dhidi ya mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ilikuwa mbinu ya kupata ushindi katika majadiliano wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.

Mwandosya alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za CCM baada ya kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho ya Mkoa wa Mbeya.

“Katika eneo kama lile ni lazima utumie lugha ambayo ilikuwa siyo nzuri kwa Tume ya Warioba ili kuweza kusisitiza jambo fulani au ni njia ya ushawishi ili kuweza kupata ushindi,” alisema Mwandosya.

“Hivyo tunapaswa kuachana na maneno na maudhi yaliyofanyika wakati ule na kufuata misingi katika kuhakikisha tunapata katiba mpya kwa masilahi ya wananchi wetu.”

Alipoulizwa kuhusu Bunge hilo kutozingatia maoni ya wananchi kwa kuondoa vipengele vilivyokuwa katika Rasimu ya Katiba, alisema kuwa maoni ya wananchi yaliyotolewa, hayakuwa kura ya maoni.

Mwandosya alitetea kuwa katika vikao vya Bunge hilo hawakuwa na rasimu yoyote ambayo waliitumia katika kutafuta Katiba Mpya, zaidi ya ile iliyoandaliwa na Tume ya Warioba.

“Hapa naomba nifafanue vizuri kuwa hatukuwa na Rasimu yoyote ambayo tuliitumia nje ya Rasimu ya Jaji Warioba na ndiyo hiyo itakuja kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana,” alisema.

Kuhusu kuondolewa kwa vipengele ambavyo vinawapa wananchi nguvu ya kuwawajibisha viongozi wao, Mwandosya alisema wamefuatilia katiba zote duniani na kugundua kuwa wananchi wana haki ya kuwawajibisha wabunge wakati wa uchaguzi mkuu. Alisema wabunge wengi wamekuwa wakishindwa kwenye chaguzi kwa kuwajibishwa na wananchi.


Chanzo:Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad