Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nianze kwa kukuuliza wewe mzazi; unapoweka picha ya mtoto wako kila hatua tangu akiwa mchanga hadi anaanza kutembea na kuanza shule, alikuomba au ulipata ruhusa yake?

Ingekuwa wewe umepigwa picha bila idhini yako halafu ukaikuta kwenye mtandao utafurahi?

Najua unampenda mtoto wako na ana haki zake za msingi pamoja na kuheshimiwa faragha yake popote alipo. Haiwezekani chochote anachofanya ukiweke kwenye mtandao.

Naomba kueleza madhara yanayoweza kutokea kwa kuweka picha za mtoto wako au wa mwenzako kwenye mitandao hasa mitandao ya kijamii kama facebook , instagram na mingineyo.


Kwanza fahamu kuwa kampuni karibu zote za mitandao ya kijamii zimesajiliwa Marekani, chache zimesajiliwa Ulaya na Asia, lakini karibu zote zinatumia sheria na sera za mataifa hayo.


Katika mataifa hayo wanasisitiza mtoto asijiunge kwenye mitandao ya kijamii hadi atakapofikisha miaka 13, wengine miaka 15 au 16 .


Kampuni zote za mawasiliano zina utaratibu wa kuhifadhi kila kitu kinachotokea kwenye shughuli zao za kila siku kwenye chombo maalumu cha kuhifadhi taarifa za mtandao (server). Kwa hiyo ukiweka picha za mtoto zinahifadhiwa huko hata kama utazifuta.


Hapo awali, nilisema mtoto anahitaji faragha yake, unaporusha picha za mtoto wako kwenye hii mitandao au mawasiliano yoyote, unaingilia faragha yake na huko mbele anaweza kukushtaki wewe au wengine walioingilia faragha yake.


Mtoto anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano .


Umeshawahi kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu kwenye mitandao hasa ya kijamii ? unajua ni kwa nini ?


Kwa sababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na ndugu zake.


Kama ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na ‘mabazazi’ kwa sababu ya picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja akabakwa.

Kwa hisani ya mwananchi tunapata elimu

Hoja yangu:
Kwanini hii tabia imezuka sana wanandoa siku hiyo hiyo mama anaugulia maumivu badala ya baba kumhangaikia mama na mwanae yeye anafuta kamera iko wapi tena siku hizi mchina amerahisisha anamfotoa mtoto na kupost kwenye wall yake ili iweje? kwamba watu wajue na wewe ni kudume cha mbegu au una kizazi? matokeo yake ndo wazazi mnapotofautiana na marafiki zenu mnawatukana mpaka watoto, kuna wengne sijui mtandao gani yule dada anauza pichu anamtukana mtoto wa mwenzaje eti baboon hivi mnahisi watoto wanajisikiaje? unamharibia mtoto future yake bila kujua, ukifikiri ni fahari kuweka picha ya mwanao sijui facebook, twitter, instagarma na kwingne huko ni ushamba na ujinga, labda siku hizi kwa kuwa imekuwa issue sana kupata mtoto but is not fair

Nawasilisha hoja
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad