Kinachoendelea Kuhusu Kesi ya Mauaji ya Mwigizaji Lulu Michael

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Musa Mateja
KESI ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi za mauaji mahakamani, Risasi Mchanganyiko limetonywa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa tena Februari mwakani kutokana na mlolongo mkubwa wa kesi za mauaji zilizopo Mahakama Kuu ya Tanzania.

Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya kamati ya majaji wanaoshughulikia kesi hiyo, kimenyetisha kuwa kesi ya Lulu itakuwa ngumu kusikilizwa wakati huu kwani mbali na wingi wa kesi mahakamani hapo, lakini pia majaji na mawakili watakwenda likizo.

“Ujue kesi ya Lulu ilikuwa miongoni mwa ambazo zingesomwa kabla ya mwaka huu kuisha, ila kulingana na vikao vya majaji inaonyesha wazi kabisa mwaka huu itakuwa ngumu hata Januari haitawezekana kwani wana kesi kama tatu za mauaji na baada ya hapo watakwenda likizo sambamba na mawakili kwani nao ndiyo kipindi chao cha likizo,” kilisema chanzo chetu.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, Aprili 7, 2012  maeneo ya Vatican-Sinza jijini Dar.Kifo cha Kanumba kilichotokea nyumbani kwake, kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
GPL
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad