Diamond Aanika Sababu Tano Kumpenda Zari The Lady Boss

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Na Nyemo Chilongani
Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.

Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.

MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.

“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji kujitangaza zaidi.”

MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari ambaye ni mama wa watoto watatu ana msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’ wengine aliwaowahi kuanguka nao dhambini.

“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na msichana asiyekuwa na msisimko wa kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na mwanamke mwenye umbo kama la mwanaume, utapata msisimko gani hapo? Lakini mcheki mtoto alivyong’aa, anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa karibu yake tu utagundua kwamba umekaa na msichana mwenye mvuto ambaye kila wakati atakufanya kuwa bize kumwangalia.”

BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni kwamba mwanadada huyo yupo vizuri kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu ziweze kupiga hatua sina budi kukaa karibu na mfanyabiashara mwenzangu (Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara ziende vipi. 

“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara, kuwa karibu naye naamini nitajifunza mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je, nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo ningeipata vipi?”

UZURI
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno yangeanza kusikikasikika na isingekuwa poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara, kumtumia kama msaada wa kunitangaza, lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza kusema kwamba haujawahi kukutana na mwanamke mzuri kama yeye.

ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa maana ya kujitambua tofauti na wanawake wote aliowahi kutembea nao.

“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti lakini kwa Zari, ni mwanamke mwenye hekima na anajitambua sana. Si mzungumzaji kivile na huwa anapenda kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili yake ameielekezea kwenye fedha zaidi. Hapendi masihara na fedha, anapenda kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda mwanamke wa hivyo kwa kuamini kwamba atanifanya nijitume zaidi.”

AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za warembo wakali Bongo aliowahi kutoka nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, aliwachambua mmoja baada ya mwingine na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini hawamfikii Zari.

UTAMBULISHO KESHO DAR LIVE
Mbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa huyo alidai kwamba atamtambulisha rasmi kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala jijini Dar atakapokuwa anaangusha burudani ya kibabe katika Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme mwenzake, Mzee Yusuf na wakali wengine kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= kwa kawaida na shilingi 20,000/= kwa V.I.P.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baada ya miezi mi3 ya kubanjuka, ukapime afya yako kwanza, maana habari nyepesi nyepesi zinasema kuwa huyo dada 'anangoma'

    ReplyDelete
  2. hana jipya ufuska ndio anaojisifia

    ReplyDelete
  3. hana jipya ufska ndio anaojisifia

    ReplyDelete
  4. Kabla hujafa hujaumbika, hao unaowaponda ndio waliokutoa ushamba na kama si wao usingekuwa na huyo Zari.

    ReplyDelete
  5. Eti ooh Diamond anafatwa na mademu kwa pesa zake tu,mara Diamond ana sura mbaya,mara nini nini nini.Sasa huyu Zari,aka,boss lady,aka,mke wa rais,aka.mtoto mzuri .......................
    anafata nini?

    ReplyDelete
  6. huyu msenge habari zake kubwa ni kuhusu mademu, mademu cyo ishu cku hizi dogo, watakumaliza hao, pumbaf, na atakaye mtetea nae ni pumbaf

    ReplyDelete
  7. Kijana mjinga sana huyu na muongo hatareee, hamjui vizuri huyo Zaituni Kirigwajo aliyejibadilisha jina na kujiita Zari. Biashara ya Joketi (ambaye anasema wana maumbo kama wanaume yeye na Penny na Wema) inajulikana ana brand yake, je huyu Zari biashara yake anaijua? Mumewe ni Don wa magang ya madrugs, yeye atafute sifa tu iko siku tutamsahau kama Bosslady wa Bongo yule Model, aliwahi kusikia wapi biashara ya Uganga wa kienyeji inamtajirisha mtu mpaka afungue mashule.

    Anyway Zari ndio anamfaa maana ni limbukeni na Mburula mwingine ambae hakumaliza hata form 4 akaishia kutafuta pesa kwa wanaume. Halafu aache kusema uongo nenda Uganda akafanye Concert kama wenzie kina Mr Nice walivyowahi kufanya au kama anavyofanya Chameleon kwenye uwanja wa wazi sio kwenye kumbi za Bar halafu aje ajisifie hapa eti nyomi watu walijaa? Walijaa kwa ukumbi wa kufanyia Party ndio unajisifia? Akafanye concert watu wajae kama kwenye fiesta ndio tumuone mwanaume kweli. Mwanaume ana mdomo mrefu kama mwali wa Kizaramo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwacheni yeye anajua utamu upo wapi

      Delete
  8. Mwacheni jamani yeye mwenyewe ana jua utamu upo wapi

    ReplyDelete
  9. Amakweli haujafa hauja umbika ivi uyo mshenzi anayo anayoyangea yanamuonesha tu kma hana akilinzuri.yeye niwakuachafua ivo walomfungua macho iyo yote anatakakuakasirikisha 2.roho inamuuma saaana kuona ka achwa kila siku alikua akimtapa wema leo anamuona mbaya uyo mbwa mkosi.

    ReplyDelete
  10. Uyo pumbafu diamond mchafu mbwa wewe leo unaweza ukayatamka ayo ayoyote yanaoneshatu kama bado unawapenda.kama ulikua ukilala nao ukiwaskia kama wanaume kwanini ulikua ukiwarudilia inamahanisha yakwamba nawewe uko shoga.mbea sutwa mwanaume kama binti.

    ReplyDelete
  11. UKIMWI baba kapime tu.Zari mgonjwa

    ReplyDelete
  12. Kupanga ni kuchagua kama ameamua kuwa na Zari nyinyi kiawauma nini? Kwani hao akina Penny, Wema na Joketi si wao ndio waliomuacha? hata kama yeye ndie aliyewaacha kwani walikuwa mume na mke si na wao kuna kitu walikifuata kwa Diamond. Mbona wewe hawakufuati? Kilamtu anao uhuru wa kuamua hatma yake mradi havunji sharia. Ila kumbuka mkono mtupu haulambwi.

    ReplyDelete

Top Post Ad