Kuwa na Wapenzi wengi kunapunguza uwezekano wa kuugua Tezi Dume

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chuo kikuu cha Montreal, Canada, ni kuwa mwanaume ambaye ameshiriki tendo la ndoa na wanawake kuanzia ishirini na kuendelea ni nadra sana kuugua ugonjwa wa Saratani ya Tezi dume.

Lakini kwa upande wa wanaume mashoga, wao wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu. Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hii kwa mashoga ni kuwa wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata maumivu kwenye tezi dume kutokana na msikusuko unaotokea wakati wa tendo pindi wanapokuwa wanafanya mapenzi haya (athari zipo kwa muingizwaji).

Kati ya mwaka 2005 na 2009 wanaume wapatao 3208 walishiriki utafiti uliofanywa na Taasisi inayojishughulisha na maradhi ya Saratani na kati yao wanaume 1590 waligundulika kuwa na Saratani hii ya Tezi dume.

Utafiti huu ulichapishwa kwenye Jarida la "Cancer Epidemiology".

Marie-Elise Parent, aliyeongoza jopo la watafiti alisema kuwa hii isiwe sababu ya wanaume kuhamasika kuwa na wapenzi wengi.

Pia utafiti huu umeweka wazi kuwa wanaume ambao hawashiriki kabisa tendo la ndoa wako kwenye hatari, mara mbili zaidi ya kawaida kuugua gonjwa hili hatari.

Tafiti zilizotangulia pia zilitanabaisha kuwa kufanya mapenzi mara kwa mara kunapunguza uwezekano wa kuugua Saratani ya Tezi Dume kwa kuwa husaidia kupunguza mrundikano wa wadudu visababishi vya Saratani (carcinogenic crystal-like substances) kwenye tezi dume.

My Take:

Kwa wanaume: Je mwenendo wako unakuweka hatarini au kwenye usalama dhidi ya Tezi dume?
Wamama na wadada, ukiombwa tunda ujue mwenzio anahitaji kinga dhidi ya Saratani. Hivyo msiwe wachoyo.
Na kidume ukiona kila unapoomba tunda unakataliwa basi ujue mwenzio anataka uugue tezi dume.

Kinga ni bora kuliko tiba.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. aixee ni majanga mwanzo mwisho.

    ReplyDelete
  2. Unanusurika kuugua TEZIDUME unadumbukia katika UKIMWI, sasa chagua kipi afadhali!

    ReplyDelete
  3. Je si unawapigia debe waliouguwa tezi dume kuwa sio waasherati?Sio ukweli tunajua watu wengi ambao wana mamia ya wapenzi na wanaugua tezi dume!

    ReplyDelete

Top Post Ad