Miss World na uhalisia Wake, Kamati ya Miss Tanzania Wanacho cha Kujifunza?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa mara ya kwanza nimeamua kuangalia mashindano ya Miss World lengo likiwa kujua ni wasichana wa aina gani wanaenda huko na vitu gani hasa wanavipa kipaumbele. Ukweli usiopingika ni kwamba shindano hili limejikita sana kwenye personal abilities mfano talents, uwezo wa kufanya kwa vitendo matendo ya kuhudumia watu/jamii wanaokuzunguka/inayokuzunguka au unaowawakilisha (huduma kwa nchi yako), practical problem solving skills, namna mrembo ameinspire vijana wenzake (kwa vitendo) na kwenye uwezo wa kujieleza.

Ni beauty with purpose na talents. Physical appearance imechukua nafasi ndogo sana. (mfano Miss sudan kusini wa mwaka huu alikuwa wakawaida kabisa ila alifika top 10, kenya alikuwa wa kawaida pia ila top 10 alifika kwa kujihusisha na kuihudumia jamii) Hii imenifanya kuyathamini mashindano haya kutokana na kwamba kumbe nchi ikiwa na muwakilishi mwenye upeo na sifa husika anaweza kuibadilisha jamii kwa kiwango kikubwa sana kwani kuna kampuni kubwa nyuma yake inayomuwezesha kufanikisha haya. 

Mfano mzuri ni Miss India wa mwaka 1994 ambaye ameweza kushinda tunzo mbalimbali za kimataifa na kuwezeshwa kutekeleza shuhuli za maendeleo ya jamii kimataifa na kitaifa. 

Kulingana na ambavyo haya mashindano yanaendeshwa kitaifa hapa Tanzania kamwe hatutaweza kushinda. hii ni kutokana na ukweli kwamba vigezo vya kimataifa havizingatiwi rushwa imewekwa mbele, wanaangalia zaidi muonekano na si pamoja na upeo wa hali ya juu, hawaangalii mshiriki ameigusa vipi jamii kwa vitendo na talents zake (huenda talents wanaangalia ila si serious sana), shindano linaonekana la kihuni sana kulingana na waandaji kutokuwa serious na kuzingatia maadili ya kazi, na pia kubebana. 

Ninakiri kwamba Miss world ni nafasi nyingine ambayo kama Tanzania itaamua kuitumia vizuri uwezekano wa kuchangia kwenye juhudi za kuuondoa umasikini kwa kugusa jamii kubwa ya watanzania unawezekana. Fursa hii itatumika tu pale ambapo kamati ya miss tanzania kuanzia vitongoji itakuwa makini kwenye kuwapata washiriki na kuepukana na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa ujumla. 

kama ambavyo diamond anaitangaza tanzania kimuziki, Miss world ni sehemu nyingine ya kuitumia ipasavyo kwani ni njia nyingine tunayoweza kuitumia kugusa jamii na kupunguza umasikini uliokithiri. 

Mwisho Mashindano haya sio uhuni (kama ambavyo wengi wanayachukulia) bali waandaaji ndio wanafanya tuyaone ni ya kihuni kwa kutozingatia vigezo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nice post! Katika siku umeongea point hii ni mojawapo< nimependa sana

    ReplyDelete
  2. Admin. ulichokisema hata Kamati ya Miss Tanzania wanakisema kila siku na wanakijua ajabu najiuliza kila siku kwanini hawakifanyii kazi.

    ReplyDelete
  3. Hakika hapa umenena lililo la Busara!

    ReplyDelete
  4. Wanatafuta mabwana tuu ndio maana lundenga ana wake wawili wote kawapata miss TZ!

    ReplyDelete

Top Post Ad