Nitamuunga mkono Mbowe Kuhusu Ufisadi wa Bomba la Gesi Gharama Kuzidishwa Mara Mbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mh.Zitto Kabwe 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Zitto aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.

“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la gesi. Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alisema Zitto.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bara hili maendeleo, hmmm itakuwa kuyasikiaga tu na kuona kwenye nchi za wenzetu, huko kwa watu wanajielewa kama wao ni binadam sio wanyama,

    ReplyDelete

Top Post Ad