TFF wakubali Coutinho kuichezea Taifa Stars Kwa Masharti Haya Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Mohammed Mdose

BAADA ya kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, kuonyesha nia yake ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemkubalia lakini limempa masharti ya kufuata.




Coutinho aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alitamka kuwa kutokana na nafasi finyu ya yeye kuichezea timu ya taifa ya nchini kwao, basi yupo tayari kuichezea Taifa Stars kama TFF itamhitaji afanye hivyo.

Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema kuwa hakuna kifungu chochote ndani ya shirikisho hilo kitakachomzuia kuichezea Stars, lakini anatakiwa kwanza kubadili uraia na siyo shirikisho kuhangaika kumbadilishia.

“Sisi hatumzuii ila kama anahitaji hivyo inatakiwa yeye mwenyewe abadili uraia na siyo sisi kumbadili, kingine pia kocha wa timu ya taifa, Martin Nooij ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho kama akishabadili atutaarifu ili tufahamu, kama kocha akivutiwa na kiwango chake na akichaguliwa basi tumjumuishe kwenye kikosi,” alisema Mwesiga.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu jamaa anataka kutuletea utani Watanzania. Hivi ni kweli Watanzania tumekosa mchezaji mzawa ambaye anaweza kuimiliki vyema nafasi ya kiungo mpaka tufikie kuchukua majeshi ya kukodiwa. Na kama ni kweli hilo litafanyika basi itakuwa kweli ni balaaa.

    ReplyDelete
  2. Mdau juu kama huyu coutinho atabadili uraia kuwa mtanzania basi anahaki zote kuiwakilisha bongo na wala sio majeshi ya kukodi tafadhali rudi shule japo ngumbaru

    ReplyDelete
  3. NCHI NYINGI ZINA FANYA HIVYO, HATA HISPANIA UNAYOIFAHAMU INA FANYA VIZURI KATIKA RECORD ZAKE WANA WACHEZAJI KUTOKA BRAZIL

    ReplyDelete

Top Post Ad