AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
BAADA ya kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, kuonyesha nia yake ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemkubalia lakini limempa masharti ya kufuata.
Coutinho aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alitamka kuwa kutokana na nafasi finyu ya yeye kuichezea timu ya taifa ya nchini kwao, basi yupo tayari kuichezea Taifa Stars kama TFF itamhitaji afanye hivyo.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema kuwa hakuna kifungu chochote ndani ya shirikisho hilo kitakachomzuia kuichezea Stars, lakini anatakiwa kwanza kubadili uraia na siyo shirikisho kuhangaika kumbadilishia.
“Sisi hatumzuii ila kama anahitaji hivyo inatakiwa yeye mwenyewe abadili uraia na siyo sisi kumbadili, kingine pia kocha wa timu ya taifa, Martin Nooij ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho kama akishabadili atutaarifu ili tufahamu, kama kocha akivutiwa na kiwango chake na akichaguliwa basi tumjumuishe kwenye kikosi,” alisema Mwesiga.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Huyu jamaa anataka kutuletea utani Watanzania. Hivi ni kweli Watanzania tumekosa mchezaji mzawa ambaye anaweza kuimiliki vyema nafasi ya kiungo mpaka tufikie kuchukua majeshi ya kukodiwa. Na kama ni kweli hilo litafanyika basi itakuwa kweli ni balaaa.
ReplyDeleteMdau juu kama huyu coutinho atabadili uraia kuwa mtanzania basi anahaki zote kuiwakilisha bongo na wala sio majeshi ya kukodi tafadhali rudi shule japo ngumbaru
ReplyDeleteNCHI NYINGI ZINA FANYA HIVYO, HATA HISPANIA UNAYOIFAHAMU INA FANYA VIZURI KATIKA RECORD ZAKE WANA WACHEZAJI KUTOKA BRAZIL
ReplyDelete