Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake na Mtangazi Gadner G Habash

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SWALI: Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?

JIBU :
Hatujaachana niliamua kumuacha

SWALI: Kwanini umeachana/umemuacha mume?

JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo, ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

SWALI: Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?

JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini.

Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao; niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso!

SWALI: Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

SWALI: Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. When i say never, I mean Never.

SWALI: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU : Nilidhani angebadilika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

SWALI: Uliwezaje kuondoka?

JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dada anajua kujibu vzr no comment hapo

    ReplyDelete
  2. Yule jamaa nimlevi mbwa nakumbuka sikumoja tupo baaflani alifanya vitu vyakijinga paka uliokaa pembeni roho inauma

    ReplyDelete
  3. Ndoa ya kikristo inakiapo kigumu sana teba sana....jarb kukaa na watu wazima wa mama ambao mpaka leo wapo na wenza wao.ujue namna walijifanya wajinga ili kuinusuru ndoa na kle kiapo kuwa

    .MPAKA KIFO KITUTENGANISHE....ni neno rahc kutamka il utekelwzaj wake ni mgumu ajarb kutafakar c

    ReplyDelete
    Replies
    1. we ni kubwa jinga kwahiyo mpaka UKIMWI ummpate afe ndio mmumsifie kuwa kalinda ndoa. Huyo anayetoka inje ya makubaliano ya ndoa yeye jukumu lake ni nini? fikra dume na dhiki zinawasumbua wanawake ndio maana mnabaki kwenye ndoa kisa mlo

      Delete
  4. polee.....wanaume wapo wengi dada....kizuri ulichosema ni.kuwa makini ktk kuchagua next tym

    ReplyDelete
  5. Nijuavyo Jaydee na Gardner hawakufunga ndoa kanisani bali Bomani.Kwa hiyo talaka ni option halali ya kuachana japo kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba aliamua kuondoka nyumbani bila kuaga.

    ReplyDelete
  6. Msisahau jamani zile nyimbo,cjui machozi,nalazimisha furaha nk..hpo G hajaongea akija naye ana yake ataongea kwaiyo hayatuhusu.,kifupi navyojua mwanaume ndie anachagua yupi aishi nae anaempenda.,mwanamke anaejiamini halazimishi kuolewa na mwanaume anaye mtaka yeye ikiea hivyo lazima atumie gharama hasa ya pesa ili kumpata,hapo ndio tatizo kwa G na J km hamjui.,mapenzi sio pesa leo analia hasara aliyoipata mwanzo hakuyasema haya zaidi ya.,wanaume km mabinti,Mara usiusemee moyo.,sass Tulia usitumie gharama kumpata unayemtaka tumia gharama kwa aliye kupenda nawe ukamtii app utafaulu,kuolewa sasa bado tulia uctafute kujionyesha eti uwezi kosa mwanaume sivyo watakuumiza Tu.,mi naamini yupo ulieahidiwa na Mungu wakufanana nawewe sio komwili. ulikuwa na haraka na sasa acha haraka tulia.,nitafute nikushauri mdada Jide Maombi muhimu Sana eneo hilo msna ndoa sio fasheni.,sikupi pole mama nafasi unayo tengeneza njia zako Yesu atende......

    ReplyDelete

Top Post Ad