Utata Mtoto wa Flora, Mbasha Amtaka Flora Amuogope Mungu na Kueleza Watu Ukweli Ulio Moyoni Mwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU chache baada ya kuibuka utata mkubwa juu ya kichanga cha kike cha mwimba Injili maarufu Bongo, Flora Mbasha huku mitandao ya kijamii ikieleza kwamba baba wa mtoto huyo si aliyekuwa mume wa mwanamuziki huyo, Emmanuel Mbasha ‘Ima’, familia ya mwanaume huyo inadaiwa kufanya kikao kizito jijini Dar ili kupata ufumbuzi, Ijumaa Wikienda linakujuza.


Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Mbasha, familia hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita nyumbani kwa Ima, Tabata-Kimanga, Dar ili kulizungumza suala hilo na kuona kama wanaweza kukubaliana kukilea kichanga hicho endapo ni damu yao.
“Ndugu walitofautiana, kila mtu alikuwa na mtazamo wake hivyo wakaona bora wakutane na kutafuta jibu la pamoja kama wanalea au hawalei,” kilisema chanzo hicho.

KIKAO CHAVUNJIKA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana ndugu hao kutofautiana kimisimamo kwani kila mmoja alitoa mawazo yake.

MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha ambaye sasa anatamba na Wimbo wa Haribu Mipango ya Shetani ambao inadaiwa amekuwa akiutumia kama kijembe kwa Flora, alisema aachwe kwanza kwani suala hilo linamuumiza kichwa na ni la  kifamilia zaidi.
“Naomba mniache kwanza, sipo vizuri kwa sasa,” alisema

CLIP YAONESHA MSIMAMO
Kwa mujibu wa ‘clip’ ya sauti yake (Mbasha) aliyoituma kwa Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye ana mtoto mmoja tu, Elizabeth Emanuel Mbasha ’Liz’ ambaye ana miaka kama kumi na moja.
Mbasha alisema hajui nini kinaendelea na kwamba ameambiwa habari za Flora kujifungua mtoto wa kike lakini yeye haoni kama habari hizo zinamhusu sana!

MSIKIE
“Mimi sijui niseme nini? Nimeambiwa kwamba Flora amejifungua. Kwa hiyo? Mbona yeye Flora hajaniambia, si anajua taarifa hizo hazinihusu? Amuogope Mungu, yeye angewaambia watu ukweli.”
Ijumaa Wikienda: “Kwa hiyo unataka kusema mtoto si wako?”
Mbasha: “Yeye anajua.”

NDUGU WA MBASHA
Ijumaa Wikienda lilizungumza na ndugu mmoja wa Mbasha (jina lipo) ambaye alizungumzia sakata la shemejiye kujifungua mtoto akiwa mbali na nyumbani:
“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.

KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mara baada ya ugomvi wao na kuondoka nyumbani miezi saba iliyopita, Flora aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akikiri kuwa na ujauzito na kusema: “Ndiyo nina mimba lakini siyo ya Gwajima.”

AZUNGUMZIA UNDUGU WAKE NA GWAJIMA
Hata hivyo, hivi karibuni, Flora alikazia tena maneno yake kwa kusema kuwa Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ni anko (mjomba) wake kwa hiyo watu wajaribu kuliangalia hilo, hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi  na mjomba‘ake.

KUHUSU MADAI KUWA MTOTO NI WA GWAJIMA
Mwanasheria: “Kwanza nataka kusema kwamba, chombo chochote cha habari ambacho kiliandika habari ya kumchafua Flora tutakishitaki. Iwe ni magazeti iwe ni mitandao ya kijamii. Wanaosema ni mtoto wa Gwajima ndiyo wanaomchafua Flora kwa sababu si kweli.”
GPL

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. D.N.A.
    Kelele za nini? wapumbavu.

    ReplyDelete
  2. Mbasha na mkewe wote wajinga,hivi kwani mkikaa kimya badala ya kuchafuana si inapendeza zaidi?Dunia ya leo kuna mtu kusingiziwa mtoto kweli?Au nyie wenzetu mko dunia gani?Mnajidharirisha tu,

    ReplyDelete
  3. Mkiona inawaumiza kichwa kaleteni matokeo ya DNA

    ReplyDelete
  4. Katika mahojiano Flora aliwahi kusema moja ya sababu zinazomfanya asitake kumsamehe Mbasha na kurudi kwake ni kumdhalilisha kijinsia( KUMWINGILIA KINYUME NA MAAUMBILE).Je hiyo inaweza kuwa sababu ya mbasha kukataa mtoto ya kwamba alikuwa anamwingilia kinyume kitu ambacho Mke asingeweza kuwa na mimba?Maana kama kweli na wewe Mbasha unamuogopa Mungu hakuna sababu ya kukataa mtoto ili hali hamjaenda kwenye Vipimo( DNA).Hakuna Mungu hapo,nyie ni mashetani maana mnaendekeza kazi ya shetani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AHAAA HIVI KWELI FLORA ULIINGILIWA KINYUMBE NA MAUMBILE NA MUMEO?????????? KWELI KWELI HASA??EMANUEL UMETENDA HAYO?????? JAMANI!!!!

      Delete

    2. Alitamka Flora mwenyewe,kwa masikio yangu nilisikia sio kuambiwa na mtu mdau,inashangaza wengi kama kuna ukweli.

      Delete
    3. DAH MDAU INANIPA SHIDA KUAMINI KAMA NI KWELI EMANUELI ALIYATENDA HAYO KWA MKE WAKE!!! AU NDIO ILE AKUFUKUZE HAKUAMBII TOKA!!! HALAFU KWANI FROLA HAKUWA NA MAHALI PA KUPELEKA MALALAMIKO YAKE AU PA KUMSHITAKI EMANUEL MPAKA AYASEME HAYO KWENYE VYOMBO VYA HABARI?? TENA KUUELEZA UMMA MAMBO YAO??? ANA MUDA GANI NA EMANUEL INA MAANA SIKU ZOTE HIZO AMEKAA NAYE MCHEZO HUO ULIKUWEPO?? AU IMANUEL AMEUNZA GHAFULA?? MWENZENU SIPATI PICHA KABISAAA. FLORA SEMA UKWELI !!!!

      Delete
    4. Kwa mtu mwenye kumtii Mungu ni ngumu sana kuamini jambo hili,na hasa ukiwaangalia hawa MBASHA'S walivyokuwa, na kuonyesha mapenzi Kwa Mungu.
      Flora anadai alikuwa anaogopa kusema kwa kuwa alikuwa anatishiwa kuuwawa,swali, mbona kasema sasa tena kwenye vyombo vya habari,ina maana haogopi kufa sasa hivi?Haipendezi kwa jamii na kwa Muumba wetu.Tuwaombee sana wawili hawa,kwa Mungu hakuna gumu.

      Delete
    5. ndio hapo miye napata utata na hilo!!! kwa hali ya kawaida flora huwezi kusema ulitishiwa maisha!!! kwani wewe mtoto mdogo? Jamani miye siamini kabisa kabisa sio kweli bwana. nina ndoa zaidi ya miaka 10 nafikia eti mungu wangu adai nyuma nikatae anitishie maisha?? nami nikubali ?? kama ni kweli walifanya kwa ridhaa sasa kumetokea ugomvi ndo anajifanya alitishia kuniua.Flora kuwa mkweli!! katika hili miye sikubaliani naye!!!

      Delete
  5. hata kama mtoto si wa mbasha au wa gwajima. si flora katiwa au kazaa je?
    so bb wa mtoto yupo

    ReplyDelete
  6. kwa kweli shetani yuko kazini. haya mambo walitakiwa wayafanye watu wasiomjua Mungu.mbona mnamtengenezea mtoto roho ya kukataliwa? huyo ni malaika jamani. hata huyo binti yenu mwingine anawaelewaje maana kawa mkubwa na anasoma magazeti. jamani frola na mbasha hebu fungeni vinywa vyenu tumechoka na upuuzi wenu. sio nyie tu wenye migogoro pia wenzenu wanayo lkn wamenyamaza.

    ReplyDelete
  7. flora na mbasha hamjui mnamtesa mtoto wenu kisaikolojia. hasemi tu ila anaumia sana.mnapanda mbegu mbaya kwa watoto wenu. pigeni magoti mwombe Mungu awape roho wa hekima awaongoze mnatia aibu sana jamani. japo waandshi wa habari na nyie mnatia chumvi sana habari.

    ReplyDelete
  8. UJOMBA SIO TIJA UNAWEZA KUZAA NAYE

    ReplyDelete
  9. flora ni mungu yupi unayemheshimu ?? maana mungu anasemehe wewe inakuacje usisamehe? dhambi zenu zijapokuwa nyekundi kama damu nitazisafisha nanyi nitakuwa weupe kama theluji. haya wewe ni kipi unashindwa kumsamehe mbasha?? SAMEHENI NANYI MPATE KUSAMEHEWA NA BABA WA MBINGUNI.kama huwezi kusamehe mbasha basi usitegemee na wewe utasamehewa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. MAOMBI ZAIDI YANAIHITAJIKA WATU WA MUNGU JUU YA WATU HAWA!!

    ReplyDelete

Top Post Ad