Kesi Yangu imenifundisha Mengi, Nilikuwa Nipo Tayari kwa Adhabu Yoyote– Chidi Benz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rapper Chidi Benz kwa sasa ni mtu huru baada ya Alhamis hii kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tisa. Amelipa faini hiyo.

Akizungumza leo kwenye ‘You Heard’ ya Clouds FM, Chidi amesema amejifunza mengi kupitia kesi hiyo.

Nimejifunza kwa sababu kuna maisha halisi ambayo nimeishi kati hapo na matatizo. Ni maisha ambayo yamebadilisha sehemu kubwa sana ya maisha yangu,” amesema Chidi. “Kwanza watu wote wanafahamu tukio hili lilinitokea na nimemalizana nalo. Pia sijaisumbua mahakama, nilikubali kwamba ni kweli nimekutwa na hivyo vitu na ni kweli nilikutwa navyo na nikikataa ni sawa sawa na ujinga kwamba adhabu ni lazima nitapewa tu. Nilikuwa nipo tayari kwa adhabu yoyote,” ameongeza.

“Unajua mimi nimefanya tukio ambalo limeonekana ni tatizo kubwa sana kutokana na unajua sisi tunaishi na maadui kuna maadui wengine wanatengeneza suala lako kuonekana kubwa sana. Kwahiyo hakimu kaangalia huyu amekosea na amekubali anaweza akawa mfano kwa wengine. Kwahiyo watu wengine wajifunze na wajiweke sawa na wasafiri.”

Chidi amedai kuwa ni mama yake ndiye aliyeilipa faini hiyo.

Mama yangu mzazi na rafiki yangu siwezi kumtaja, watu wawili tu ndo walikuwa pamoja na mimi. Mama yangu mzazi ameshughulikia kila kitu, faini pesa kulipa kila kitu kafanya yeye mama yangu mzazi. Kwahiyo mama yangu mzazi pekee ameshughulikia, namshukuru sana.”

We all have life storms, and when we get the rough times and we recover from them, we should celebrate that we got through it. No matter how bad it may seem, there's always something beautiful that you can find.
By Mattie Stepanek

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chid ww ni staa mkubwa sana ctaki kuamini eti ulikuwa Huna laki tisa hapo ulipo hadi mama yako na rafiki yako wajichange ndo wakulipie!!!

    ReplyDelete
  2. MTOTO KWA MAMA HAKUI BIG UP MAMA CHID!! SO CHID RUDISHA FADHILA KWA MAMA MTUNZE NA KUMJALI KWA SAANA. NA ZAIDI YA YOTE ACHA KUTUMIA MADAWA HAYO!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad