Mahabusu Afia Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki baada ya Kujitundika na Kunyinyonga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Picha si ya Tukio hilo
Mahabusu mmoja Shabani Ramadhani (28), amekutwa amejinyonga katika choo cha Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki, jijini Dar es Salaam.



Tukio hilo lilitokea jana baada ya mahabusu huyo kufikishwa katika kituo hicho juzi akituhumiwa kufanya tukio la unyang’anyi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alijinyonga kwa kutumia kamba ya kaptura aliyovaa.

Kamanda Senga alisema marehemu alijinyonga alfajiri katika choo wanachokitumia mahabusu hao na mwili wake kugundulika nusu saa baadaye.

“Alikwenda chooni kati ya majira ya saa tisa na saa kumi alfajiri wakati wenzake wakiwa wamelala na ndiko alikojinyongea kwa kutumia kamba ya kaptura yake, lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Senga.

Mama mdogo wa marehemu ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa  Ramadhani alikamatwa na Polisi Ijumaa iliyopita na kufikishwa katika kituo hicho akiwa salama.

Alisema jana walifika katika kituo hicho kwa ajili ya taratibu za kumwekea dhamana, ndipo walipoelezwa kuwa ndugu yao amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba.

“Sisi wenyewe tunashangaa iweje kajinyonga wakati tunavyofahamu mtuhumiwa anapofikishwa polisi anatolewa vitu vyote alivyonavyo na kuingizwa mahabusu?,” alihoji mama huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. AM SO SAD.. ameamua kujinyonga coz no sheria hapa nchini.....nawachukia police watanzania from bottom of my heart...hawawasikilizi kabisa wananchi yan weng wamekua mahakimu... wakat hawaruhusiwi kuhukumu...na dhamana ni bure but police bila pesa utok

    ReplyDelete

Top Post Ad