Askofu Gwajima Atakiwa Kujisalimisha Kituo cha Polisi Haraka Kujibu Tuhuma za Kumtukana Askofu Pengo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na:
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MHH...KIMENUKAA

    ReplyDelete
  2. Angemtukana Imam ndio KINGENUKA HALAFU KIKANUKIA!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEE ACHA VIASHIRIA VYA UDINI. VIBAYA!!!

      Delete
  3. huyu si bure mapepo yake yanamrudia..m2 mwenye akili timamu hawezi kuongea maneno mabaya vile halafu mtumishi gani wa Mungu analindwa na walinzi haaa haaaa ifiike kipindi waumini jmn muangalie na sehemu za kuabudu khaaa..huyu ni chizi maneno yake ya ovyo eti mtumishi wa Mungu khaaaa

    ReplyDelete
  4. Gwajima msanii komedi, hafai hata kuchambia

    ReplyDelete
  5. Mlivyomtesa Mbasha Sasa yanawarudia. Chezea malipo ni hapahapa.

    ReplyDelete

Top Post Ad