Mlinzi Dr. Slaa, Akanusha Kutaka Kumuua, Adai CHADEMA Wana Chumba Cha Mateso, Aonyesha Alivyopigwa na Kuumizwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mlinzi wa DK Slaa
Aliyekuwa mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya chama hicho.

Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari leo, amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.

Amesema kutokuelewana kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho kulianza pale alipoanza kupishana kwa maneno kati yake na mke wa Dk. Slaa ambapo Slaa alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa Dk. Slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya Jumamosi aliitwa Makao Makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuta vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke, kumtesa, kumvua nguo, kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha CCM ili amuue katibu mkuu dk. Slaa.

“Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii, tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”

“Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa Slaa kwa muda wa miaka mingi sana, tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki” amesema Kagenzi

Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefichua mipango ya kitesaji na kigaidi inayofanya na CHADEMA huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.

“Jamani hiki chama ambacho kina ndoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia? Maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu na kuweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote, eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma, jamani nawaambia mimi hanitumi mtu” ameedelea kusema Kagenzi.

Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .

Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.

Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa

Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawahi kupokea pesa hizo.

Hatua atakazochukua

Kagenzi amesema hatua iliyobaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubiri kesi mahakamani ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya kiuaji.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UCHUNGUZI UFANYWE KWA HILI

    ReplyDelete
  2. UCHUNGUZI UFANYWE NA KAMA KUNA UKWELI WATANZANIA WAJULISHWE ILI WASIJE IWEKA NCHI HATARINI NA NINAWEZA KUAMINI KUWA YAWEZEKANA KUNA UKWELI MAANA HUYU MTU HAWEZI KUSINGIZIA JAMBO KUBWA KIASI HICHO....CHUNGUZENI MTUJUZE PLS

    ReplyDelete
  3. Tulisema slaa n mtu hatar mkabeza....vumilia

    ReplyDelete
  4. Slaa hafai hata kwa kurumagia, apeleke ukabila wake huko Chadema

    ReplyDelete
    Replies
    1. ACHA UJINGA WEWE?? MARANDO MCHAGA? ZITTO MCHANGA? MNYIKA MCHANGA? LISSU MCHANGA? WEWE NDO HUFAI KABISA

      Delete

Top Post Ad